• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Brentford wasajili kipa Alvaro Fernandez kutoka Uhispania

Brentford wasajili kipa Alvaro Fernandez kutoka Uhispania

Na MASHIRIKA

BAADA ya kupiga Arsenal 2-0 katika mchuano wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu, limbukeni wa kipute hicho Brentford wamemsajili kipa Alvaro Fernandez wa Huesca kwa mkopo.

Brentford waliopandishwa ngazi kushiriki EPL mwishoni mwa msimu uliopita wa 2020-21 kwa mara ya kwanza tangu 1947, watakuwa huru kurefusha mkataba wa mlinda-lango huyo kwa miaka mitano zaidi kufikia mwisho wa msimu huu wa 2021-22.

Fernandez, 23, anatua kambini mwa Brentford baada ya kuongoza timu ya taifa ya Uhispania kuzoa nishani ya fedha kwenye Olimpiki zilizopita za Tokyo, Japan mwaka huu.

Katika kampeni za Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) msimu uliopita wa 2020-21, Fernandez aliwajibishwa na Huesca mara 22 na akakosa kufungwa bao katika michuano mitano.

Amewakilisha Uhispania katika mashindano mbalimbali ya kiwango cha chipukizi kabla ya kujumuishwa katika kikosi kilichovaana na Lithuania kirafiki mnamo Juni 2021 kwa ajili ya kujiandaa kwa fainali za Euro.

Brentford almaarufu The Bees, watakutana na Crystal Palace katika mchuano wao ujao wa EPL ugani Selhurst Park mnamo Agosti 21, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Linda Katiba wasema waliopendekezwa kuteuliwa makamishna wa...

WANDERI KAMAU: Tukomeshe unyama huu kwa vijana wa Kenya