• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
CCM yajizolea asilimia kubwa ya viti uchaguzi wa mitaa uliosusiwa na Chadema

CCM yajizolea asilimia kubwa ya viti uchaguzi wa mitaa uliosusiwa na Chadema

Na AFP

DAR ES SALAAM, Tanzania

CHAMA tawala nchini Tanzania (CCM) kimeshinda zaidi ya asilimia 99 ya viti ambavyo upinzani ulisusia kwa madai ya kudhulumiwa na kutishwa, kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa Jumatatu.

Kura iliyopigwa Jumapili ililenga viti 16,000 vya viongozi wa mitaani na vijiji; nyadhifa ambazo ni muhimu mno katika maisha ya Watanzania.

Chama tawala cha tangu jadi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Rais John Magufuli kilifagia kura jinsi ilivyotarajiwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Chadema, chama kikuu cha upinzani, kilisema mapema Novemba kwamba hakitashiriki kwa kuwa wagombea wake walikuwa na hofu kuu au walikuwa wamerushwa nje kutokana na sheria kali.

Vyama vingine vitano vidogo pia vilijiunga na hatua hiyo ya ususiaji.

“Katika maeneo mengi, wagombea wa CCM hawakuwa na ushindani wowote,” Waziri wa Usimamizi wa Kimaeneo na Serikali nchini humo, Selemen Jaffo, alieleza vyombo vya habari Dodoma.

Akaongeza: “Katika sehemu chache mno, wagombea wa upinzani walishinda kwa sababu hawakuwa wamejiondoa rasmi kugombea.”

Viongozi nchini humo huwa na mamlaka makubwa Tanzania.

Kwa mfano, wazee huhitaji idhini kutoka kwa chifu wa eneo lao ili kuweza kupata huduma ya afya bila malipo.

Katika uchaguzi wa awali mnamo 2014, CMM ilishinda robo nne za viti 12,000 vilivyokuwa vikiwaniwa mwaka huo. Chadema ilichukua asilimia 15.

Chadema inasema wanaharakati wao wametekwa nyara na kupigwa huku kadha wakitoweka na kisha kupatikana wakiwa wameuawa.

Mgombea kuchaguliwa moja kwa moja

Katika jiji kuu la Dar es Salaam, vituo kadha vya kupigia kura vilifungwa kwa sababu mgombea wa CCM alisimama bila kupingwa na hivyo akachaguliwa moja kwa moja.

Maeneo manne miongoni mwa maeneo 26 makuu ya Tanzania hayakushiriki uchaguzi huo kamwe baada ya upinzani kususia.

Wachanganuzi wa siasa wanasema chaguzi hizo nchini humo huenda zikaashiria hali itakavyokuwa mwaka ujao, wakati Rais John Magufuli, kiongozi imara ambaye amekuwa mamlakani tangu 2015, anatarajiwa kugombea tena.

Magufuli ameshutumiwa vikali na mashirika ya uangalizi kutokana na rekodi yake kuhusu haki za kibinadamu.

Vyombo vya habari huru vimetiwa hofu na sheria kali kuhusu uhalifu kidijitali, magazeti na blogu za wakosoaji zimenyamazishwa huku wanaharakati wa upinzani wakihangaishwa.

  • Tags

You can share this post!

Hofu Bandari kwa matokeo duni, sasa waita mkutano

Mwili wa aliyejirusha baharini kutoka kwa feri wapatikana

adminleo