• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
CDF Francis Ogolla amuomba Rais Ruto msamaha kwa kusahau kumtambua Mama wa Taifa

CDF Francis Ogolla amuomba Rais Ruto msamaha kwa kusahau kumtambua Mama wa Taifa

NA CHARLES WASONGA

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Nchini (KDF) Jenerali Francis Ogolla mnamo Jumamosi, Oktoba 14, 2023, aliungama kwamba alivunja itifaki wakati wa sherehe za Siku ya KDF katika Kambi ya Kijeshi ya Embakasi Garrison kwa kufeli kumtambua Mkewe Rais William Ruto, Rachel Ruto.

Hata hivyo, Jenerali huyo alitambua dosari hiyo haraka na kumwomba msamaha Rais Ruto.

“Kabla ya kukualika Mheshimiwa Rais, ningetaka kuomba msamaha. Nilipokuwa nikitambulisha waliohudhuria, niligundua kuwa sikutambua Mheshimiwa Mama wa Taifa. Naomba radhi kwa dosari hiyo,” Ogolla akasema na kugeuka kuangalia jukwaa la rais kisha kupiga saluti.

Rais Ruto na mkewe walikuwa wageni wakuu wakati wa sherehe hizo zilizoandaliwa katika kambi hiyo iliyoko eneo la Embakasi, Nairobi, kuwakumba wanajeshi waliotenda vitendo vya kijasiri vitani.

Alipoanza kusoma majina ya waliohudhuria, Jenerali Ogolla alianza kwa kumtambua Rais kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini (KDF), Waziri wa Ulinzi Aden Duale, Spika wa Seneti Amason Kingi, Mawaziri, Makatibu wa Wizara, Naibu Mkuu wa Majeshi, Makamanda wa Vikosi vya Wanajeshi, wanajeshi wa kawaida na wale waliostaafu miongoni mwa wengine.

Rais Ruto na Mkewe Rachel waliwaongoza wanajeshi wengine wa KDF kuweka shada la maua kwa heshima ya wanajeshi waliukufa wakiwa kazini.

Wake (wajane) wa wanajeshi hao waliokuwepo katika hafla hiyo pia walipewa nafasi ya kutoa heshima zao kwa kuweka shada la maua kwenye mnara maalum wa ukumbusho.

Siku ya KDF imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tangu Oktoba 2012 baada ya Kenya kutuma wanajeshi wake nchini Somalia katika Operesheni Linda Nchi kupambana na Al Shabaab mnamo Oktoba 2011.

Kauli mbiu ya sherehe za mwaka huu ilikuwa ni: ‘Jeshi Moja Wajibu Mmoja wa Kuendeleza Usalama wa Kitaifa na Kikanda’.

  • Tags

You can share this post!

Serikali kukwamua vyuo vikuu kwa ufadhili wa Sh90 bilioni

Ruto awapongeza wanajeshi wa KDF kwa kulinda nchi dhidi ya...

T L