• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 PM
City Mortuary kuzindua makafani maalum ya matajiri

City Mortuary kuzindua makafani maalum ya matajiri

Na WINNIE ONYANDO

SERIKALI ya Kaunti ya Nairobi imetangaza mpango wa kufungua tawi maalum la chumba cha kuhifadhi maiti cha City, litakalotumika na mabwanyenye.

Mpango huo kulingana na Gavana wa Kaunti, Bw Johnson Sakaja unalenga kusaidia makafani ya City kupata ushindani na vyumba vingine vya kibinafsi vya kuhifadhi maiti ambavyo vina umaarufu na wateja wengi.

Tawi hilo litakuwa na idara ya huduma kwa wateja kwa uhusiano wa wateja na vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kushughulikia miili 24 kwa wakati mmoja.

Pia, itakuwa na kanisa na huduma zingine za mazishi kama vile gari la kubebea maiti na kifaa cha kuteremsha jeneza kaburini.

Kulingana na Afisa Mkuu wa Afya ya Umma, Tom Nyakaba, hatua ya serikali ya kaunti kufanikisha mpango huo ni sehemu ya juhudi za utawala wa Gavana Sakaja kuboresha utoaji huduma katika sekta ya afya.

“Pamoja na Afisa Mkuu wa vituo vya afya Geoffrey Mosiria, tumewasiliana na mwanakandarasi husika kuhakikisha kuwa vifaa vyote hitajika vinapatikana ili kuimarisha utoaji huduma katika sekta hiyo. Chini ya uongozi wa Bw Sakaja, tutahakikisha kuwa wale ambao wamepoteza wapendwa wao wanahudumiwa kwa heshima,” akasema Bw Nyakaba.

  • Tags

You can share this post!

Joshua Arap Sang apendekeza Eric Omondi apelekwe kituo cha...

Miili ya watoto waliosombwa na mafuriko yapatikana

T L