• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:55 AM
Congo yajifua kubaki ligini, Buruburu ikilia maamuzi ya refarii

Congo yajifua kubaki ligini, Buruburu ikilia maamuzi ya refarii

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

KOCHA wa Congo Boys FC, Abdulnassir Kassim ameutaja ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Buruburu Sports mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa wa matumaini katika kupigana vita vyao vya kutaka kubakia katika ligi hiyo.

Kassim aliambia Taifa Leo Dijitali kuwa wataendelea kupambana kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Liberty FC katika mechi watakayocheza ugenini na kumaliza na Gor Mahia uwanja wa nyumbani ili kuhakikisha wanajinasua kutoteremshwa ngazi.

“Tungelishginda kwa mabao mengi dhidi ya Buruburu lakini washambulizi wangu walishindwa kutumia nafasi nyingi walizopata za kufunga na hasa katika kipindi cha kwanza. Lakini namshukuru Mungu kuondoka na pointi tatau,” akasema Kassim.

Katika mechi hiyo, Congo Boys ilijipatia mabao hayo mawili yaliyotingwa nyavuni ni Anwar Abdulhakim kwa mkwaju wa penalti dakika ya 37 na Hussein Abdulmalik kunako dakika ya 53.

Mkufunzi huyo anasema katika mechi za hivi karibuni, amekuwa akiwapa chipukizi nafasi ya kucheza ili waweze kupata uzoefu na kufanikiwa kuinua vipaji vya uchezaji wao kwa kujitayarisha kwa ligi ya msimu ujao.

“Nawapa fursa hii chipukizi wangu kwani nataka wawe na uzoefu wa kutosha wa kuweza kukabiliana na wapinzani katika ligi ya msimu ujao. Nina furaha kuwa wanafanya vizuri ninapowapa nafasi hiyo,” akasema Kassim.

Kwa wakati huu, Congo Boys iko kwenye nafasi ya 14 kati ya timu 16 zinazoshriki ligi hiyo ikiwa na pointi 32 hali timu nyingine ya Pwani ya Young Bulls FC iko nafasi ya 13 kwa kuwa na alama 34 sawa walizo nazo Kangemi iliyoko nafasi 12 lakini ina mabao zaidi.

Wakati huo huo, kocha wa Buruburu Sports, Patrick Orwako ametoa ombi kwa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) liwe likiangazia zaidi mechi za kumaliza msimu kwani kumekuwa na matatizo ya marefarii kuzisaidia timu za nyumbani.

Akitoa ombi hilo akiongea na wanahabari baada ya kushindwa mabao 2-0 na Congo Boys FC, Orwako alitaka FKF isiwapange waamuzi kwenye mechi zinazohusisha timu zao za nyumbani akidai huwa kuna mapendeleo.

“Ninasikitika kuwa japo vijana wangu wamejituma na kucheza kwa kujitolea, lakini walivunjwa nguvu na baadhi ya maamuzi ya refarii na hivyo kutufanya tuondoke kiwanjani tukifikiriwa kuwa tumeonewa,” akasema mkufunzi huyo.

Alisema hata wachezaji wamekuwa na fikra ya kuwa ni afadhali kutosafiri na kutoa ushindi wa bwerere kwa kufahamu haina maana ya kwenda ugenini wakati marefarii wamekuwa tayari kuchezesha kuhakikisha timu za kwao zinapata ushindi kwa njia zozote zile.

Aliwasifu wachezaji wake kwa kuweza kufanya safari zao ingawa wamekuwa na changamoto kadhaa tangu msimu uanze na akaomba wadhamini wajitokeze kuwasaidia ili msimu ujao wafanye vizuri.

  • Tags

You can share this post!

UEFA: Vipusa wa Chelsea na Arsenal wafahamu wapinzani wao...

Avokado husaidia hasa wanawake kuyeyusha mafuta tumboni...