• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Daddy Owen afunguka kuhusu uhusiano wake na Charlene Ruto

Daddy Owen afunguka kuhusu uhusiano wake na Charlene Ruto

NA RAJAB ZAWADI
IKIWA umekuwa mwenyeji wa jijini huenda ulizisikia zile taarifa kwamba staa wa nyimbo za injili alirusha ndoano ya mapenzi kwa bintiye Rais William Ruto, na chambo kikagonga ndipo.

Taarifa hizo ziliibuliwa na Nairobi News, mojawapo ya safu zinazomilikiwa na Shirika la Habari la Nation (NMG), ambayo iliripoti kuwa staa huyo kwenye hekaheka za kuelekea sherehe za Krismasi 2023, Desemba 23, kimya kimya aliibuka kijijini kwao Eshifiru kumtambulisha Charlene Ruto kwa mamake mzazi Margaret Mwatia.

Babake Daddy alifariki dunia 2017

Utambulisho huo unasemekana haukuwa wa kishikaji ila ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msela kuja kumposa mwanawe wa tatu wa Rais Ruto.

Baada ya taarifa hizo kutoka, imeishia kuibua hisia kem kem kila mmoja akijijazia ya kwake huku Charlene na Daddy wakiamua kucheza chini licha ya vyanzo kibao kuthibitisha kufanyika kwa tukio hilo ambapo wengine tayari wameshalitaja kuwa kama ni ‘nikah‘ vile.

Hata hivyo, baada ya kusukumwa sana, Daddy Owen amefunguka kuhusu tukio hilo na hasa zaidi aina ya mahusiano yaliyopo kati yake na Charlene ambaye miezi ya hivi karibuni wamekuwa kama vile ni mapacha, hawaachani, hawapishani.

“Naomba tusiende huko, naelewa watu wana maswali kibao maana nimekuwepo kwenye tasnia ya Showbiz kwa miaka 20 kwa hiyo naelewa watu wangetaka kujua sana. Ila bwana haimaanishi kwamba kila nikionekana na demu eti lazima kuwe na la ziada,” Daddy Owen kafunguka. Tetesi za kuwa Daddy na Charlene ni mtu na mpoa wake kwa sasa, zilianza katikati ya 2023.

Alipohojiwa kuhusu ukaribu wake mnamo Novemba, msela aliruka stori akisisitiza kwamba wao ni washikaji tu na kinachowaweka karibu ni kazi zao za kijamii ambazo wamekuwa wakishirikiana kuzitekeleza.

Sababu kubwa ya taarifa hizi kuzua hisia kibao, zinatokana na kwamba kando na mtoto wa Rais kuhusuka, pia ile sakata ya Daddy Owen kukimbiwa na mke wake wa miaka sita 2020 bado inazua kumbukumbu kwa wengi.

Faridah Wambui aliamua kumtoka msela baada ya jamaa kusota kwa mujibu wa habari zilizotoka kipindi akimwacha Daddy kwa mataa.

 

  • Tags

You can share this post!

Wanajeshi 1, 000 wa Burundi walitumwa kisiri mashariki mwa...

Ufanisi dhidi ya pombe haramu Mlima Kenya ilikuwa hekaya tu?

T L