• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 AM
Daraja bovu lililojeruhi watu 16 mtaa wa mabanda lakarabatiwa

Daraja bovu lililojeruhi watu 16 mtaa wa mabanda lakarabatiwa

Na SAMMY KIMATU

BAADA ya ‘Taifa Leo’ kuangazia daraja moja lililojeruhi watu 16 katika mtaa mmoja wa mabanda wa Mukuru, Kaunti ya Nairobi  sasa limekarabatiwa.

Mafundi walifanya kazi usiku wote wa kuamkia jana wakichomelea vyuma na likorogea simiti na kokoto.

Lilifungwa kwa shughuli hiyo hadi saa saba za mchana wa jana Jumatano kwa ufadhili waa mwakilishi wa wadi ya Landi Mawe, Bw Herman Kaimosi Azangu.

Daraja la kuvukia kwa miguu la Mukuru/Kaiyaba linalounganisha mitaa ya River Bank Phase I na Phase 2, South B lilikuwa katika hali mbaya kwa muda mrefu.

Lilitengenezwa mwaka 2002 na aliyekuwa rais wa Baraza la Ngumi za Madola (Commonwealth Boxing Council) na aliekuwa mbunge wa Makadara, Bw Reuben Ndolo.

Kufikia wiki jana watu 16 walipata majeraha ya miguu walipoingia ndani ya mashimo na kujeruhiwa na mabati ya vyuma.

“Watu walikuwa wakikatwa na mabati miguu ikiingia ndani ya mashimo baada ya vyuma vilivyokuwa vimetandazwa chini kuchipuka, kuoza na kung’oka,” Bw Humphrey Mudogo akasema.

Bw Humphrey alisema miongoni mwa waliojeruhiwa ni pamoja na mzee wa umri wa miaka 70.

Vilevilem watoto watatu waliokolewa kutoka ndani ya mto Ngong baada ya kuteleza walitembea juu ya daraja lenyewe.

Akiongea Jumatano, Bw Azangu alisema fauka ya daraja kuwahudumia wakazi kutoka wodi yake, huwasaidia pia wanaofanya kazi katika Eneo la Viwanda sawia na kuunganisha kituo cha biashara cha South B.

“Singesubiri mpaka tupoteze maisha juu ya daraja duni. Nimejitolea kusimama na wananchi katika kupata suluhu ya kudumu kwani ni bora kukinga kuliko kuponya,” Bw Azangu asema.

Kadhalika mwanasiasa hiyo alijitolea kukarabati daraja zingine tano zote zikiwa katika mpaka wa wodi ya Landi Mawe na ya Nairobi Kusini.

Daraja hizo ni pamoja na la Commercial/Fuata Nyayo, Kenya Wine/Brightstar (Kanaro), Kaiyaba/Hazina, Maasai Village/Express na Shimo La Tewa/ South B.

You can share this post!

Maafisa wawili wa gereza wakamatwa na DCI kuhusu kifo cha...

Matayarisho ya Olimpiki yanoga Japan

adminleo