• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Eric Omondi aenda Uingereza na kugeuka ombaomba barabarani, akifanikiwa kuchangisha Sh340, 000 kununulia unga Wakenya wanaolala njaa

Eric Omondi aenda Uingereza na kugeuka ombaomba barabarani, akifanikiwa kuchangisha Sh340, 000 kununulia unga Wakenya wanaolala njaa

NA SAMMY WAWERU

MCHEKESHAJI Eric Omondi amesababisha gumzo mitandaoni kufuatia hatua yake kugeuka ombaomba jijini London, Uingereza katika kile anahoji ni kufanya mchango kuokoa Wakenya wanaoteseka njaa.

Video inayosambaa mitandaoni, msanii huyo ameonekana katika mojawapo ya barabara London akiomba pesa.

Bw Eric ametetea hatua hiyo akisema lengo lake ni kulisha raia wa Kenya wanaolala njaa, kufuatia gharama ya juu ya maisha.

Kupitia video hiyo, amefichua amefanikiwa kuchangisha kima cha Sh340, 000 barabara mbalimbali jijini London.

Watu walionekana wakimchangia, katika moja ya mtaa wenye shughuli nyingi London.

Eric alikuwa na kibango kilichoandikwa: “Tafadhali saidieni, mambo ni mabaya. Mabaya zaidi.”

Msanii huyo alidai mchango huo utatumika kununulia unga Wakenya wanaohangaika.

“Wakiomba tunaomba…Nikiwa Uingereza, nilitenga muda kuchanga pesa katika mitaa mbalimbali London ambazo zitatumika kusaidia Wakenya kwa sababu ni kubaya. Nilifanikiwa kuchangisha Sh340, 000, fedha ambazo nitatumia kununulia Wakenya wachache unga,” Bw Eric alisema.

Pesa zitakazosalia, mtunzi huyo wa kontenti za kimitandao alidokeza kwamba zitatumika kusaidia kuinua wasanii wenza.

Alisema atawanunulia vipakatalishi (laptops) kuboresha kazi zao.

Jitihada zake, hata hivyo, zilizimwa na maafisa wa polisi London.

Eric vilevile alilalamikia ubaguzi wa rangi, kupitia utangamano wake na baadhi ya wananchi Uingereza.

Ziara ya msanii huyo Uingereza ilijiri baada ya matamshi ya Waziri wa Biashara, Bw Moses Kuria kudai kujutia kufadhili safari ya kwanza ya Eric Omondi nchini Amerika.

Eric alisema ziara ya London ilipania kuthibitishia Waziri Kuria kuwa kwa sasa anamudu maisha ya raha mustarehe.

Kuria alifadhili msanii huyo maarufu kuenda Amerika miaka saba iliyopita.

Eric Omondi aidha anapinga kutozwa ushuru (VAT) watunzi wa machapisho ya mitandao (kontenti), kwa minajili ya biashara, akihimiza Waziri Kuria kuzungumza na Rais William Ruto kuwapa vijana muda wajijenge.

Mswada tata wa Fedha 2023 uliopitishwa Jumatano, Juni 14, 2023 unapendekeza nyongeza ya VAT kwa bidhaa muhimu za kimsingi na pia biashara.

 

 

 

 

  • Tags

You can share this post!

Polisi walaumiwa kwa kufumbia macho masaibu ya wasichana wa...

Gathoni Wamuchomba asifiwa kwa kupinga Mswada wa Fedha

T L