• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Handiboli: Handege yalipua Mang’u High

Handiboli: Handege yalipua Mang’u High

NA LAWRENCE ONGARO

MABINGWA watetezi wa mchezo wa handiboli Mang’u High walisalimu amri ya Handege Secondary ya Gatundu iliyowazima 25-21 katika fainali kali ya mashindano ya shule za kanda ya Kati iliyopigiwa M-Pesa Foundation mjini Thika, Ijumaa.

Katika semi fainali Handege iliichapa GeaceLand kwa mabao 32-22. Mang’u High iliigonga Leshan kwa mabao 29-14.

Katika mashindano ya handiboli ya wasichana, Shule ya Nyathuna (Kiambu), ilihifadhi ubingwa wao kwa kuilipua Muthithi Girls 24-10.

Katika semi fainali Nyathuna iliichapa Shamata (Nyandarua) mabao 24-13. Nayo Muthithi (Murang’a) iliigonga Kinale Girls (Kiambu) mabao 26-18.

Mabingwa watetezi wa vikapu kwa wasichana Loreto waliicharaza M-Pesa Foundation kwa vikapu 26-13.

Hapo awali katika semi fainali Loreto ikishinda Karima kwa pointi 51-36. Halafu M-Pesa Foundation iliichapa Magomano (Nyandarua) kwa vikapu 74-41.

Nayo Thika High ndio mabingwa wapya wA vikapu kanda ya Kati kwa kuigonga Mang’u High kwa 53-42.

Katika fainali ya magongo, mabingwa watetezi Mang’u High walisalimu amri ya Gaichanjiru kwa kulimwa bao 1-0.

Katika mchezo wa magongo kwa wasichana, mabingwa watetezi Loreto Girls waliicharaza M-Pesa Foundation kwa mabao 3-2.

Katika fainali ya raga, Mang’u High waliigonga Alliance kwa 10-3.

Katibu wa michezo ya shule kanda ya Kati Virginia Murage amesema timu zote zilizoibuka nafasi ya kwanza kwa wavulana na wasichana zitasafiri  mjini Eldoret Aprili 23 hadi 27 kushiriki michezo ya kitaifa.

Alisema wakufunzi wote kutoka shule tofauti walijitahidi pakubwa kuwaandaa wanafunzi hao waliyoshiriki michezoni.

  • Tags

You can share this post!

Mashindano ya riadha kanda ya Kati yatia fora licha ya mvua

Rubani asifiwa kwa kuzuia ajali licha ya mshtuko wa nyoka

T L