• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 5:55 AM
Huduma Centre ya Thika sasa kuhudumia wananchi kuanzia alfajiri

Huduma Centre ya Thika sasa kuhudumia wananchi kuanzia alfajiri

NA LAWRENCE ONGARO

KITUO cha Huduma Centre mjini Thika, kimebadilisha sura ya utendakazi kwa wananchi.

Meneja wake Bi Sharon Nzau, alisema kutokana na wateja wao kuwa wengi wamebadilisha saa zao za kuwahudumia.

“Kutokana na wingi wa wateja wetu tumebadilisha saa za kazi ambapo tunafungua afisi zetu mwendo wa saa kumi na mbili unusu za alfajiri na kufunga jioni saa moja unusu za jioni,” alisema Bi Nzau na kuongeza hata wateja wetu wanafurahia huduma zetu.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa wateja wanaohudumiwa wameridhishwa na utenda kazi wa kituo hicho.

Alisema mafanikio hayo ni kwa sababu kila kitu hapo ni kupitia mitandao ya kidijitali na kazi kufanyika haraka kabisa.

Ilidaiwa hapo awali wananchi waliteseka kwa kupiga foleni ndefu lakini kwa sasa mambo ni rahisi kwa kila mwananchi.

Alisema hali ya usalama katika eneo hilo umeimarishwa vilivyo ambapo kamera za CCTV zimetundikwa kila sehemu ili kuweka kila kitu kwa hali njema.

Kwa siku moja imethibitishwa kuwa wateja 1500 hadi 2,000 kupokea huduma katika kituo hicho.

Baadhi ya huduma zinazotolewa hapo ni kupata kadi ya hospitali ya NHIF, KRA, HELB, kitambulisho cha kitaifa na hata cheti cha kuwa na tabia njema.

Bw Jeff Mwangi aliyefika kupata kitambulisho kipya cha kitaifa alisema ameridhishwa na utendaji kazi katika kituo hicho.

“Ninafurahia huduma tunayopokea kutoka hapa kwani baada ya dakika 20 hivi kila kitu huwa kimekamilika,” alisema Bw Mwangi

Bw Denis Oloo afisa mkuu wa usalama alisema kuwa hatua ya serikali kuleta huduma karibu na mwananchi ni cha kushabikiwa kwa sababu kila mmoja hupata huduma bila ubaguzi wowote.

You can share this post!

Makahaba watua Kiambu kunyonya Sh1.6 bilioni za fidia kwa...

Shujaa wa vita dhidi ya ukeketaji katika jamii ya Wamaasai

adminleo