• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:55 AM
Kakamega Homeboyz yamwajiri kocha John Baraza

Kakamega Homeboyz yamwajiri kocha John Baraza

NA JOHN ASHIHUNDU

KLABU ya Kakamega Homeboyz imemteua John Baraza kama kocha wake mkuu kujaza nafasi ya Benard Mwalala aliyetimuliwa mara tu msimu uliopita ulipokamilika.

Tangu Mwalala aondoke, timu hiyo imekuwa ikinolewa na Edward Manoa aliyepewa usukani kama kocha mhikilizi.

Lakini jana Alhamisi klabu hiyo ilitangaza rasmi kumpa jukumu hilo Baraza, zamani mshambuliaji wa Sofapaka na timu ya taifa, Harambee Stars ambaye atasaidiwa na Peter Okidi, anayerejea.

“Nimefurahia jukumu hili jipya. Ni furaha yangu kurejea kwenye soka ya kiwango cha juu,” alisema Baraza ambaye msimu uliopita alikuwa kocha wa Mara Sugar FC ya Supa Ligi (NSL).

Baraza alijiunga na Mara Sugar msimu uliopita ukielekea ukingoni na kuisaidia kumaliza miongoni mwa 10 bora.

Alikuwa amejiunga na klabu hiyo baada ya hapo awali kunoa Equity Bank FC aliyosaidia kutinga nusu-fainali ya FKF Cup.

Hapo awali, mshambuliaji huyo mstaafu aliinoa Sofapaka kwa wakati tofauti, kama kocha msaidizi na baadaye kocha mkuu wa muda.

“Homeboyz ni timu kubwa na niko tayari kwa changamoto iliyo mbele yangu. Bilas haka tutafaulu katika malengo yetu ya msimu ujao,” aliongeza.

Homeboyza ilimaliza msimu uliopita katika nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa Tuskser, lakini kwa tofauti ya mabao baada ya kila moja kumaliza kwa pointi 66.

Baraza anachukuwa jukumu la kuinoa Homeboyza ambayo majuzi ilipoteza David Okoth na Yema Mwana waliojiunga na Kenya Police, pamoja na Sylvester Owino aliye barani Ulaya kwa majaribio.

Akizungmza na Taifa Michezo, meneja wa timu hiyo Boniface Imbenzi alisema kikosi chake kingali imara hata baada ya kupoteza mastaa kadhaa waliojiunga na timu nyingine. Wachezaji hao alisema ni pamoja na kiungo mahiri Moses Mudavadi, mwenye umri wa miaka 27.

Baada ya kupoteza nyota kadhaa, Homeboyz imewasajili Simon Abuko kutoka KCB, Eugene Wethuli na Meshack Muyonga kutoka Mathare United. Kadhalika timu hiyo imefanikiwa kumtwaa John Otieno.

Wengine waliosajiliwa ni Ibrahim Wanzala, Brian Wekesa na Mathias Isogoli.

  • Tags

You can share this post!

Hapa kazi tu, Ruto aambia mawaziri

Jinsi muungano unavyookoa msitu Samburu

T L