• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 12:45 AM
Karo: Magoha aonya walimu akiwataka kutofukuza wanafunzi

Karo: Magoha aonya walimu akiwataka kutofukuza wanafunzi

Na LAWRENCE ONGARO

WALIMU wakuu wa shule za upili wameagizwa wasiwafukuze wanafunzi kwa sababu ya karo ya shule.

Waziri wa Elimu Prof George Magoha alisema Ijumaa kwamba kwa wakati huu, ni muhimu wazazi wapewe muda wa kulipa fedha zilizosalia.

“Wakati huu sio wa kuwafukuza wanafunzi kwenda nyumbani. Wazazi wanastahili kupewa muda ili watoto wao waendelee na masomo,” alisema Prof Magoha.

Aidha, alieleza kuwa tayari serikali imesambaza Sh59.4 bilioni kwa shule za upili huku Sh15.4 zikienda kwa masomo ya shule za msingi.

Alitoa onyo kali kwa watu wanaowatunga mimba wanafunzi wa shule huku akisema watachukuliwa hatua kali na serikali.

Aliyasema hayo alipozuru Shule ya Msingi ya Mutomo iliyoko Gatundu Kusini, Kaunti ya Kiambu.

Alisema serikali itafanya juhudi kuona ya kwamba kila mwanafunazi awanapata elimubila kubaguliwa.

Alieleza kuwa chuo cha Mama Ngina kitafunguliwa rasmi Septemba 2021 ambapo wanafunzi kutoka eneo hilo pia watapewa nafasi ya kwanza kujiunga na chuo hicho.

Wakati wa ziara hiyo aliandamana na mkurugenzi wa Shirika la Ahadi Kenya Dkt Stanley Kamau, ambapo waliwakabidhi wanafunzi hao sodo, sabuni, na vifaa muhimu vya matumizi ili kukabiliana na janga la Covid-19 lakini pia kuboresha afya zao.

Dkt Kamau aliwataka machifu wawe mstari wa mbele kuona ya kwamba wanafunzi wanahudhuria shule.

“Tunajua kuna wazazi ambao bado wanaketi na wana wao nyumbani. Kwa hivyo ni jukumu la machifu kufanya uchunguzi kujua ni watoto wangapi hawahudhurii masomo,” alisema Dkt Kamau.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Kenyatta (KU) Prof Paul Wainaina.

You can share this post!

Bertrand ajiunga na Leicester baada ya kandarasi yake na...

MAINGI: Wanawake wanaowania nyadhifa za uongozi...