• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Keter akubali kushindwa na limbukeni wa siasa

Keter akubali kushindwa na limbukeni wa siasa

Na CHARLES WASONGA

WAZIRI wa zamani wa Kawi Charles Keter amekubali kushindwa na Dkt Erick Mutai katika mkuja ya mchujo iliyofanyika mnamo Aprili 14, 2022.

Kwenye taarifa fupi kupitia akaunti yake ya twitter Bw Keter pia aliwashukuru wafuasi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA), wafuasi wake washindi wote katika zoezi hilo kwa kudumisha amani.

“Nashukuru watu wa Kericho kwa kujitokeza  kwa wingi na kupiga kura katika mchujo uliokamilika. Pongezi zangu ziwaendee washindi wote. Nawatakia kila la kheri.

“Kwa wafuasi wangu, maajenti na makundi ya kampeni, niwashukuru kwa kusimama nami. Mungu awabariki na Mungu abariki Kaunti ya Kericho,” Bw Keter akaongeza.

Katika matokeo yaliyotangazwa Ijumaa jioni Dkt Mutai alishinda kwa kuzoa jumla ya kura 126,000 dhidi ya kura 60,342 za Bw Keter.

Mhadhiri huyo mwenye umri wa miaka 38 sasa anatarajiwa kushinda kiti cha ugavana wa Kericho kwa urahisi ikizingatiwa kuwa chama cha UDA ni maarufu zaidi katika kaunti hiyo ya Kericho.

Dkt Mutai ambaye ni mhadhiri wa somo la Isimu katika Chuo Kikuu cha Embu ni limbukeni katika uwanja. Hii ndio mara yake ya kwanza kuwania kiti chochote cha siasa.

  • Tags

You can share this post!

Wanjigi adai Raila ni kivuli cha Uhuru

Wafuasi watishia kuhama UDA baada ya uteuzi wa ukora

T L