• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 11:55 AM
KNBS: Asilimia 55.6 ya wakazi Kiambu wana uzani zaidi ya kilo 100

KNBS: Asilimia 55.6 ya wakazi Kiambu wana uzani zaidi ya kilo 100

NA MWANGI MUIRURI

ZAIDI ya asilimia 55 ya wakazi wa Kaunti ya Kiambu, wengi wakiwa ni wanawake, ni wanene kupindukia na wanahimizwa kutathmini lishe kando na kuanza kufanya mazoezi kupunguza uzani.

Shirika la Takwimu Nchini (KNBS) limetoa takwimu hii, likisema Kiambu watu wengi wana uzani usio wa kawaida.

Kulingana na asasi hii ya kiserikali, wengi wa wakazi katika kaunti hiyo wanazidisha kilo 100.

“Isitoshe, lishe kwa watoto imezorota vibaya sana. Wadau katika sekta ya afya ya jamii wana jukumu la dharura kuingia Kiambu na kuzindua mikakati ya uhamasisho kuhusu jinsi ya kutunza uzani katika viwango vinavyokubalika kiafya,” akasema Bw Macdonald Obudho ambaye ni afisa msimamizi KNBS.

Kwa ujumla, alisema kwamba asilimia 55. 6 ya wenyeji Kiambu wana uzani ambao sio wa kawaida na aliohoji unazua hofu.

Akizungumza katika hafla ya uhamasisho, Bw Obudho alisema kwamba Kaunti ya Kiambu ni ya maana sana katika safu za idadi ya watu na pia uchumi wa taifa “hivyo basi ikiathirika ni suala la kuzua wasiwasi”.

Msimamizi wa sekta ya afya Kiambu Bw Hillary Kagwa alisema kwamba utawala wa Gavana Kimani Wamatangi umeajiri wasaidizi wa kustawisha afya ya kijamii mashinani, na hao ndio watatumika kutoa uhamasisho huo wa kuchunga uzani.

“Tutaingia mashinani na tuanze uhamasisho hasa kwa wanawake wetu wapunguze uzani na pia lishe kwa watoto ipewe umakinifu. Gavana wetu tayari amezindua mradi wa lishe bora katika shule za msingi za Kiambu na hilo litatuokoa sana,” akasema.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Wakfu wa M-pesa msaada wa Sh79 milioni kujenga kituo cha...

Raia wa Uchina alivyosaidiwa na hakimu kuelewa mashtaka ya...

T L