• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 PM
KNCHR yaanza uchunguzi kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu wakati wa maandamano

KNCHR yaanza uchunguzi kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu wakati wa maandamano

ALEX KALAMA Na STEVEN HEYWOOD 

TUME ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya uvunjaji wa haki za binadamu wakati wa maandamano yaliyofanyika Jumatatu. 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kupitia mwenyekiti wake Roseline Odede, tume hiyo imesema inachunguza ripoti za kukamatwa kwa watu, uharibifu wa mali, majeruhi na madai ya polisi kutumia risasi za moto.

Tume hiyo, kwa kushirikiana na mamlaka huru nyingine, imesema wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu ripoti hizo. Na iwapo zitathibitishwa, litakuwa jambo lisilofaa na wanaohusika wanaweza kushtakiwa kwa msingi wa kanuni ya jukumu la uongozi.

Hata hivyo tume hiyo ya haki za binadamu imeitaka Mamlaka ya Kuchunguza Utendakazi wa Polisi (IPOA) kufanya uchunguzi huru kuhusu madai hayo.

KNCHR pia imewataka maafisa wa polisi kutotumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji, ikisema wanatumia nguvu kupita kiasi. Ingawa polisi walitangaza maandamano hayo kuwa haramu, KNHCR imesisitiza kuwa maafisa wanapaswa kufuata mwongozo wa usimamizi wa amani ya umma wakati wa maandamano.

“Viwango ni wazi sana na kwa hivyo lazima vizingatiwe kwa roho na barua kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Kenya na Maagizo ya Utumishi wa Polisi.

Maafisa wa polisi wanapaswa kuweza kuwatenga na kuwakamata waandamanaji wenye vurugu ambao wanakiuka amani na wakati huo huo kulinda wale wasio na hatia wakati wa maandamano,” amesema Bi Odede.

Walakini, tume hiyo imewaonya waandamanaji dhidi ya kutumia maandamano kuharibu mali, kuumiza wengine na kuiba, ikisema inaweza kusababisha makosa ya jinai.

“Tume itaendelea kufuatilia na kunakili  hali inayoendelea na inasisitiza kwa Wakenya kwamba haki zinapaswa kutumiwa ndani ya mipaka ya sheria na kwa njia ambayo inaheshimu haki za wengine,”  amesema Bi Odede.

  • Tags

You can share this post!

Mapenzi yanoga, Madam Boss, Akothee afichua humpigia simu...

Maandamano ya Azimio sasa kufanyika kila Jumatatu na...

T L