• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Ligi Kuu: KCB FC yapiga hatua baada ya kung’ata Rangers.

Ligi Kuu: KCB FC yapiga hatua baada ya kung’ata Rangers.

Na JOHN KIMWERE

KCB FC imecheka na wavu mara mbili ndani ya kipindi cha kwanza na kusajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Posta Rangers kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF-PL) iliyopigiwa ugani Kasarani Annex, Nairobi.

Nayo Sofapaka FC ilichapwa mabao 3-1 na Kariobangi Sharks huku mabingwa wa zamani Gor Mahia FC ikiachana sare ya bao 1-1 na Bidco United ugani Thika Stadium mjini humo. Posta Rangers ilikiri kichapo hicho na kumaliza rekodi ya mechi saba bila kushindwa.

Ushindi wa KCB ulifanya kocha wake, Zedekiah Otieno kujaa furaha huku wachezaji wake walizungumzia jinsi walivyopambana kwa udi na uvumba kuzima wapinzani wao. Makosa ya David Cheche Achieng yalichangia KCB kupata bao la kwanza dakika ya 27 kupitia Henry Onyango kabla ya Posta Rangers kuzawazisha dakika tisa baadaye kupitia juhudi zake Timothy Otieno.

Hata hivyo KCB ilipata bao la ushindi dakika moja kabla ya kipindi cha kukatika lililofumwa kimiani na Derrick Otanga. ”Nina furaha tele kwa ufanisi wa pointi tatu muhimu baada ya kushiriki mechi tatu mfululizo bila ushindi. Itabidi kukaza buti ili kukabili wapinzani wetu kwenye mechi zijazo ambapo tumekaa vizuri kufanya kweli,” kocha wa KCB alisema na kutoa wito kwa vijana wake kutolaza damu dimbani.

Maafande wa Ulinzi Starlets walishindwa kutamba mbele ya wenzao wa Maafande wa Kenya Police na kuagana sare mabao 2-2, FC Talanta ilisajili matokeo kama hayo na Nzoia Sugar FC. Katika jedwali la mechi hizo, Kakamega Homeboys ingali kifua mbele kwa alama 32, nne mbele ya Kariobangi Sharks.

Nayo KCB inafunga tatu bora kwa kusajili alama 28, moja mbele ya City Stars na Gor Mahia tofauti ikiwa idadi ya mabao.

You can share this post!

Kivumbi kikali kushuhudiwa robo fainali za Koth Biro

Vihiga Queens kileleni licha ya sare

T L