• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:55 AM
Luka Modric atia saini kandarasi mpya ya mwaka mmoja kambini mwa Real Madrid

Luka Modric atia saini kandarasi mpya ya mwaka mmoja kambini mwa Real Madrid

Na MASHIRIKA

KIUNGO raia wa Croatia, Luka Modric, 35, amezima tetesi alizokuwa akihusishwa nazo kwenye soko la uhamisho wa wachezaji msimu huu kwa kutia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja kambini mwa Real Madrid ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Modric aliingia katika sajili rasmi ya Real mnamo Agosti 2012 baada ya kuagana na Tottenham Hotspur kwa kima cha Sh4.6 bilioni.

Mnamo 2018, Modric alijizolea taji la Ballon d’Or ambalo hutolewa kila mwaka kwa Mchezaji Bora zaidi duniani.

Ufanisi huo ulimfanya kuwa mwanasoka wa kwanza mbali na Lionel Messi wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina na Cristiano Ronaldo wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno kutia kapuni taji hilo katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Modric aliongoza Croatia kutinga fainali ya Kombe la Dunia mnamo 2018 nchini Urusi japo kikosi hicho kikazidiwa maarifa na Ufaransa waliowapokeza kichapo cha 4-2.

Nyota huyo atakuwa nahodha wa Croatia kwa mara nyingine katika fainali zijazo za Euro 2020 kati ya Juni 11 na Julai 11, 2021. Croatia watafungua kampeni zao kwenye kipute hicho dhidi ya Uingereza mnamo Juni 13 uwanjani Wembley.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

KBF yakutana na kuamua ligi za mpira wa vikapu zirejee

Bayern Munich wamsajili beki Omar Richards kutoka Reading FC