• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 2:16 PM
Machozi kwa Senegal, Ghana na Cameroon katika vita vya kufuzu Kombe la Dunia

Machozi kwa Senegal, Ghana na Cameroon katika vita vya kufuzu Kombe la Dunia

CORONI, NGAZIJA:

Ghana, Cameroon, Senegal, Afrika Kusini na Zambia wamejaa kiwewe kuhusu safari ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia la mwaka wa 2026 baada ya kutupa alama muhimu katika mechi za raundi ya pili.

Ghana, ambao wameshiriki Kombe la Dunia mara nne ikiwemo 2022 nchini Qatar, waliduwazwa na Comoros (Ngazija) kwa bao 1-0 jijini Moroni, Jumanne.

Wanavisiwa wa Comoros wanaongoza Kundi I kwa alama sita wakifuatiwa na Mali (nne), Madagascar (Bukini) na Ghana (3), Jamhuri ya Afrika ya Kati (1) na Chad (0).

Afrika Kusini, ambao wameshiriki dimba hilo mara tatu na wanalenga kurejea katika jukwaa hilo baada ya kukosa makala matatu mfululizo, walinyamazishwa na Rwanda 2-0 mjini Butare.

Rwanda wamekaa juu ya Kundi C kwa alama nne wakifuatiwa na Afrika Kusini (3), Nigeria, Lesotho na Zimbabwe (2) na Benin (1).
Mabingwa wa Afrika wa 2012, Zambia, pia walipata pigo walipokung’utwa 2-1 na wenyeji Niger ugani Marrakech.

Morocco wanaongoza Kundi E kwa alama tatu. Walizaba Tanzania 2-0 Jumanne. Wako mbele ya Zambia, Niger na Tanzania kwa tofauti ya mabao, ingawa watatu hao wamesakata mechi mbili. Congo Brazzaville wako mkiani bila alama.

Cameroon wanaofukuzia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya tisa, waliponyoka na alama moja kwa sare ya 1-1 na wenyeji Libya mjini Benina.

Indomitable Lions imo kileleni mwa Kundi D kwa alama nne, sawa na Cape Verde na Libya nayo nambari tatu Angola ina tatu. Mauritius na Eswatini zina pointi moja na sifuri, mtawalia.

Teranga Lions ya Senegal inaongoza Kundi B kwa alama nne. Mabingwa hao wa Afrika walitoka sare tasa dhidi ya Togo. Sudan pia wana alama nne baada ya kubwaga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 1-0 Jumapili.

DR Congo wana alama tatu, Togo mbili nao Mauritania na Sudan Kusini moja kila moja.

Matokeo (Novemba 21):

Botswana 1-0 Guinea (Kundi G), Ethiopia 0-3 Burkina Faso (Kundi A), Lesotho 0-0 Benin (Kundi C), Malawi 0-1 Tunisia (Kundi H), Rwanda 2-0 Afrika Kusini (Kundi C), Somalia 0-1 Uganda (Kundi G), Eswatini 0-2 Cape Verde (Kundi D), Sao Tome & Principe 0-2 Namibia (Kundi H), Sudan Kusini 0-0 Mauritania (Kundi B), Mauritius 0-0 Angola (Kundi D), Comoros 1-0 Ghana (Kundi I), Togo 0-0 Senegal (Kundi B), Libya 1-1 Cameroon (Kundi D), Niger 2-1 Zambia (Kundi E), Tanzania 0-2 Morocco (Kundi E).

  • Tags

You can share this post!

Kenya kumenyana na Sudan dimba la Cecafa U-18...

Mume wangu hana ustadi wa kucheza mechi chumbani, nifanyeje?

T L