• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 1:47 PM
Malawi kutegemea idadi kubwa ya wanasoka wa ligi yao ya nyumbani kwenye AFCON 2022

Malawi kutegemea idadi kubwa ya wanasoka wa ligi yao ya nyumbani kwenye AFCON 2022

Na MASHIRIKA

MKURUGENZI wa benchi ya kiufundi wa timu ya taifa ya Malawi, Mario Marinica ametaja kikosi cha wanasoka 23 pekee watakaotegemewa na taifa hilo kwenye fainali za Kombe la Afrika (AFCON) 2022 badala ya 28 kwa sababu ya janga la corona.

Wengi wa wanasoka hao 23 ni wale wanaopiga soka ya kulipwa nchini Malawi.

Licha ya makali yake msimu huu kushuka pakubwa, mvamizi Gabadinho Mhango wa Orlando Pirates nchini Afrika Kusini ametiwa katika kikosi hicho kinachojivunia pia huduma za kipa Charles Thom, beki Lawrence Chaziya na Zebron Kalima watakaochezea Malawi kwa mara ya kwanza.

Mshambuliaji Schumacher Kuwali ametemwa kwenye kikosi hicho baada ya kupata jeraha la paja akiwa katika kambi ya mazoezi nchini Saudi Arabia. Nyota mwingine wa haiba kubwa ambaye si sehemu ya kikosi hicho cha Malawi ni mvamizi wa Al Hilal, Gerald Phiri Jr.

Malawi wametiwa katika Kundi B kwa pamoja na Guinea, Zimbabwe na wanafainali wa 2019, Senegal.

KIKOSI CHA MALAWI KWA AJILI YA AFCON 2022:

Makipa: Ernest Kakhobwe (Nyasa Big Bullets, Malawi), William Thole (Be Forward Wanderers, Malawi), Charles Thom (Silver Strikers, Malawi).

Mabeki: Lawrence Chaziya (Civo United, Malawi), Dennis Chembezi (Polokwane City, Afrika Kusini), Gomezgani Chirwa (Nyasa Big Bullets, Malawi), Peter Cholopi, Stanley Sanudi (wote wa Be Forward Wanderers, Malawi), Mark Fodya (Silver Strikers, Malawi), Limbikani Mzava (AmaZulu, Afrika Kusini).

Viungo: John Banda (UD Songo, Msumbiji), Chikoti Chirwa (Red Lions, Malawi), Chimwemwe Idana (Nyasa Big Bullets, Malawi), Micium Mhone (Blue Eagles, Malawi), Charles Petro (Sheriff Tiraspol, Moldova).

Mafowadi: Peter Banda (Simba SC, Tanzania), Yamikani Chester (Be Forward Wanderers, Malawi), Zebron Kalima (Silver Strikers, Malawi), Francisco Madinga (Dila Gori, Georgia), Richard Mbulu (Baroka FC, Afrika Kusini), Gabadinho Mhango (Orlando Pirates, Afrika Kusini), Khuda Muyaba (Polokwane City, Afrika Kusini), Robin Ngalande (St George, Ethiopia).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

TAHARIRI: Ushirikiano unahitajika mno katika elimu 2022

‘Jungle’ Wainaina aeleza jinsi Njonjo...

T L