• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
MALEZI KIDIJITALI: Athari mseto za matumizi ya dijitali kwa familia

MALEZI KIDIJITALI: Athari mseto za matumizi ya dijitali kwa familia

MATUMIZI ya dijitali yamebadilisha muundo na uhusiano katika familia na athari zake zinaweza kuwa hasi au chanya.

Haya ni kwa mujibu wa utafiti wa kina kuhusu mchango wa dijitali katika malezi na familia.

Watafiti hao wanasema digitali imesababisha mabadiliko katika mahusiano ya kifamilia huku wazazi na watoto wakizama katika teknolojia kwa mawasiliano na kazi na hivyo kukosa muda wa kujumuika ana kwa ana.

“Kukosa muda wa kujumuika kama familia kutokana na wazazi kufanya kazi kwa masaa mengi hata wakiwa nyumbani, kunafanya teknolojia kuwa njia ya kuungana na kuwasiliana ambapo inaacha pengo kubwa katika uhusiano wa wazazi na watoto na familia yao kwa jumla,” wanasema wataalamu wa malezi digitali wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uingereza.

Aidha wamebaini kuwa teknolojia inavunja muundo wa familia huku kila mtu akishughulika kivyake.

Hata hivyo wanasema ingawa hali hii inaonekana kuwa hasi kwa familia, teknolojia ya dijitali inaweza pia kutumiwa kuimarisha familia.

“Teknolojia ya dijitali ni muhimu kwa maisha ya familia katika karne hii ya 21,” wanasema watafiti na kuongeza kuwa wanafamilia wanafaa kutia bidii kudumisha mawasiliano na kutafuta muda kuwa na kila mmoja wao.

Isitoshe, wanasema teknolojia ya dijitali imesababisha talaka kwa baadhi ya wazazi na kuwa pigo kwa watoto ambao huigeukia kujaza pengo la malezi wanayokosa endapo wazazi wao wangekuwa pamoja.

“Watoto wa wazazi waliotengana wanageukia intaneti na kuitumia kukita maisha yao ya kila siku. Hatari iliyopo kwao ni endapo watakosa mtu wa kuwashauri kuepuka mitego ya wahalifu wa mitandao,” wanasema watafiti.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Kuimarisha ladha ya chapati za maji

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Morgan Freeman na Jung Kook...

T L