• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Mama mboga aliyedunga kisu mgeni aliyemvamia nyumbani ashtakiwa kwa jaribio la mauaji

Mama mboga aliyedunga kisu mgeni aliyemvamia nyumbani ashtakiwa kwa jaribio la mauaji

NA JOSEPH NDUNDA

MWANAMKE mwenye umri wa miaka 27 alikanusha shtaka la jaribio la kuua kwa kumchoma kisu mara mbili, mwanaume aliyevamia nyumba kwake, eneo la Kaloleni mjini Nairobi saa mbili asubuhi.
Faith Nyanchama Mangera anadaiwa kujaribu kuua Filbert Nzoyisaba, Desemba 2, jamaa asiyemtambua.
Afisi ya Mashtaka inamtuhumu Bi Mangera kwa kumdunga kisu Bw Nzoyisaba sehemu ya kichwa na tumboni wakati wa ugomvi ndani ya nyumba.
Mshtakiwa ambaye ni mama mbonga, alitupa kisu hicho na kupiga ripoti katika kituo cha polisi cha Makongeni na kumwacha mwathiriwa akiwa amelala nyumbani kwake.
“Polisi walifika eneo la tukio na kupata umma wamempeleka kwenye kituo cha hospitali baadaye alisafirishwa hadi Hospitali ya Mama Lucy anapoendelea kupata matibabu. Tulianza kutafuta kisu na hatukupata,” alisema polisi mmoja.
Pia, aliambia polisi alikuwa analala na wanawe wakati alisikia sauti ya kutisha kwenye lango lake, kabla ya kufahamu kilichokuwa kikijiri, Bw Nyoyisamba alikuwa ameingia ndani ya nyumba.

Alisema alipomtaka mtu huyo kujitambulisha, aliendelea kumkaribia na hapo ndipo alipomdunga kisu mara mbili na kupiga kamsa ambapo majirani waliwasili.

Kakake Nzoyisaba aliwasili katika eneo la mkasa baada ya kujulishw akuhusu kisa hicho na kumpata alishahamishwa katika hospitali ya Mama Lucy Kibaki, ambapo amelazwa hadi sasa.
Bi Mangera alikanusha mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Irene Gichobi katika Mahakama ya Makadara na kuachiliwa kwa bondi ya Sh300,000 au mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itatajwa Januari 9, 2024.

Polisi walifahamisha afisi ya upelelezi kwamba mwanamume huyo bado hajaandikisha taarifa kwa sababu bado hawezi kuongea kutokana majeraha anayouguzisha hospitalini.

Picha zake zinazoonyesha majeraha akiwa hospitalini zilitolewa kama ushahidi.

  • Tags

You can share this post!

Barua ya majonzi ya binti kwa Waziri Kindiki akimsaka...

Tumetokomeza kipindupindu, endeleeni na shughuli zenu,...

T L