• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Mapigano kati ya wanajeshi na M23 yanaendelea kaskazini magharibi mwa Goma

Mapigano kati ya wanajeshi na M23 yanaendelea kaskazini magharibi mwa Goma

NA MASHIRIKA

KINSHASA, DRC

MAPIGANO makali kati ya kati ya jeshi la Congo na M23 yanaendelea kati ya kilomita 25 hadi 70 kaskazini magharibi mwa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kwa mujibu wa Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw Stephane Dujarric, Mkuu wa ujumbe wa kulinda amani nchini DRC (MONUSCO), Bintou Keita kwa sasa yuko mashariki mwa nchi hiyo.

Bi Keita alikutana na Gavana wa kijeshi wa jimbo la Ituri mnamo siku ya Jumatano.

Bi Keita ameomba msaada wa tume ya kulinda amani kuendelea kujenga uwezo wa vikosi vya usalama vya Congo.

Isitoshe, mapema wiki hii, Bi Keita alikutana na Gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini na wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa kwa nia ya kuimarisha ushirikiano na kutatua changamoto za usalama.

Bi Keita pia alishirikiana na wawakilishi wa mashirika ya kiraia na viongozi wanawake wanaokabiliwa na changamoto katika jamii zao.

Mnamo Jumanne wiki hii, Rais wa Rwanda, Bw Paul Kagame alisema nchi yake haina uhusiano wowote na M23 akiongeza kwamba kundi hilo ni zao la ubadhirifu.

Rais Kagame alisema utawala wake haupaswi kulaumiwa kwa hali ya sasa ikiwa ni pamoja na wakimbizi kuishi nchini mwake kwa zaidi ya miaka 20.

“Tatizo la M23 lilianza mwaka 2012 na makubaliano ya kulitatua yamevunjwa kufikia mapigano yanayoendelea kufikia sasa,” alisema.

Rais Kagame alizungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Kijiji cha Urugwiro Aliongeza kwamba M23 ni moja tu kati ya vikundi 120 vilivyojihami kwa silaha na vimekithiri katika eneo la Mashariki mwa Congo.

“Mimi mwenyewe sijashutumu Rwanda kuwa imeunda M23 lakini wanaotulaumu ni kwa sababu wanatuhusisha nayo,” alisema.

Kulingana na Kagame, kuna haja ya kuangalia sababu za msingi za yale ambayo pande zote mbili zinakabiliana nayo ikiwa ni pamoja na kukataa kutekeleza makubaliano yaliyopita.

Kagame alisema Rwanda haijajihusisha na mapigano ya hivi majuzi.

“Hebu tuangalie hata hiyo mikataba ya zamani tuone ni ipi ilifikiwa na ile ambayo haikuwa na matumaini ya kutatua suala hili,” alisema Kagame.

Isitoshe, Rais Kagame alikanusha shutuma kwamba Rwanda inajihusisha na kujiongezea ardhi huku ikinufaika na madini akitaja madai hayo kuwa ya kupotosha matatizo halisi.

  • Tags

You can share this post!

Ulinzi Starlets kukabana koo na Gusii Starlets...

Majengo ya sasa si kama ya zamani

T L