• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
Masoko Nairobi na Kiambu yanayouzia wateja mbegu za avocado badala ya viazi  

Masoko Nairobi na Kiambu yanayouzia wateja mbegu za avocado badala ya viazi  

NA RICHARD MAOSI

WAUZAJI na wasambazaji wa mazao ya chakula katika masoko ya Kangemi, Githurai 45 na Uthiru wametakiwa kuwa waaminifu, baada ya kubainika kuwa baadhi yao wanachanganya viazi na mbegu za avacado.

Hali ni kama hiyo katika steji ya mabasi ya Railways na pembezoni mwa soko la Muthurwa ambapo sasa itamlazimu mnunuzi kuwa makini, asije akauziwa mbegu za parachichi zilizochanganywa na viazi.

Unapozuru maeneo husika, utakutana na vijana ambao wamepanga ndoo zilizojaa viazi wakijaribu kushawishi wateja kununua, huku wakiahidi kuwatengenezea bei.

Ann Achieng ambaye ni muuzaji wa ndizi katika soko la Kangemi, anasema biashara nyingi hapa huendeshwa katika kona zenye giza saa za jioni, wakazi wengi wanapokuwa wametoka kazini na huwa hawana muda wa kukagua viazi kwa sababu ya uchovu.

“Wanaofanya biashara ya kuchanganya viazi na mbegu za parachichi ukichunguza, utagundua sio wauzaji halisi wa soko la hapa Kangemi na hawana sehemu maalum ya kuendesha biashara zao, hivyo basi ni rahis kuwapunja wanunuzi,” Achieng akasema.

Anasema inasikitisha kuona biashara hapa zikiendeshwa katika mazingira duni ya uchafu ambapo taka huwa zimezagaa kila sehemu na sehemu kubwa haijawekewa mataa ya kumulika usiku.

Anaungama kuwa hatua moja kuboresha uaminifu ili kukabiliana na matapeli miongoni mwa wafanyabiashara, ni kuzindua mradi wa kuweka mataa ili kuboresha usalama.

Anasema kuwa baadhi ya wauzaji wanatumia fursa hii kuwaibia wanunuzi, ikizingatiwa kuwa viazi vimeadimika jambo ambalo limesababisha mfumuko wa bei ya bidhaa yenyewe.

Kwa mfano, kipimo cha awali ambacho kiliuzwa Sh50 sasa itawalazimu wanunuzi kuchimba mifuko yao zaidi hadi Sh150, huku debe la Sh350 sasa likiuzwa Sh900.

Kwa sababu ya bei ghali, viazi havinunuliki, kwa upande mwingine ada ya kusafirisha mazao kutoka shambani hadi sokoni vilevile ikipanda

Kwa mfano, ilikuwa ikigharimu mkulima Sh200 kusafirisha magunia mawili ya viazi kwa pikipiki kutoka kijijini Kagaa hadi Githinguri, lakini kwa sasa waendeshaji pikipiki wanatoza kati ya Sh450 hadi Sh500.

  • Tags

You can share this post!

Ruto apata ‘nyaunyo’ kwa jina Felix Koskei...

Masaibu ya afya: Mama asiyeshuhudia hedhi alivyojifungua...

T L