• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 AM
Masuala Manne Makuu: Raila asimama kidete

Masuala Manne Makuu: Raila asimama kidete

KIONGOZI wa upinzani, Bw Raila Odinga alisimama kidete na kusisitiza wanayotaka yatekelezwe na serikali ya Rais William Ruto.

Bw Odinga alikuwa katika mkutano na wajumbe kutoka Marekani waliokuja kwa patanisho kati ya Bw Raila na Rais Ruto.Hata hivyo, iliibuka kuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua alikataa katakata ombi lolote la Bw Raila kupewa serikali ya Nusu Mkate.

Aidha, Bw Gachagua anamtaka Bw Odinga kukomesha maandamano yanayoendelea kwanza kisha akubali mazungumzo na kutangaza kustaafu kwake kabisa kutoka kwa siasa.

Kwa upande mwingine, naye kiongozi huyo wa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya anataka serikali ikubali kujadili kile ambacho kambi yake sasa imedhihirisha kuwa ni ‘Mambo Makuu Manne’ wanayotaka yatimizwe na serikali.

Fauka ya hayo, Maafisa wa Marekani wakiongozwa na Seneta wa Delaware, Bw Chris Coons – anayesifiwa kwa kushiriki katika hafla ya hadisheki ya Bw Odinga-Kenyatta mwaka 2018 – na balozi wa Marekani, Bw Meg Whitman walikutana na Bw Gachagua mnamo Jumatano asubuhi kabla ya kukutana na Bw Odinga jioni.

“Tuliwasilisha masuala manne kwake ambayo hayawezi kupunguzwa na yanayomhusu raia. Alichukua na kusema nchi inapaswa kusalia na amani nasi tukamwambia kwamba waandamanaji wetu wataendelea kudumisha amani tunaposhinikiza matakwa yetu,” msemaji wa muungano wa Azimio, Prof Makau Mutua aliambia ‘Taifa Leo’ jana Ijumaa.

Katika mkutano huo, Bw Odinga aliripotiwa kuionya serikali ya Rais wa Marekani Joe Biden dhidi ya juhudi zozote za kuunga mkono kile alichokitaja kuwa kuibuka kwa ‘ugandamizi’ nchini.

Kadhalika, katika mikutano na Bw Odinga, Seneta Coons anaripotiwa kuelezea wasiwasi wake kuhusu jinsi hali ya siasa imeathiri uchumi wa nchi na kuwaomba wanaAzimio kusitisha maandamano hayo.

  • Tags

You can share this post!

Mbarire ataka maandamano ya Azimio yazimwe

Bunge laidhinisha hoja kukarabati Coast General

T L