• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 3:17 PM
Matunda ya Gachagua kuboresha sekta ya kahawa yaanza kuonekana, mkataba kuuza zao Ubelgiji ukiiva

Matunda ya Gachagua kuboresha sekta ya kahawa yaanza kuonekana, mkataba kuuza zao Ubelgiji ukiiva

JAMES MURIMI na DPCS

WAKULIMA wa kahawa nchini wanasherehekea baada ya Naibu Rais Rigathi Gachagua kufanikisha makubaliano ya kuuza zao hilo moja kwa moja kwa kampuni kubwa zaidi ya kahawa duniani, The Java Coffee Company.

Bw Gachagua alitia saini mkataba huo na kampuni hiyo iliyoko Rotselaar, Ubelgiji Ijumaa, Oktoba 27, 2023.

Katika mkataba huo, Kampuni ya Kahawa ya Java, iliahidi kununua kahawa ya Kenya moja kwa moja kutoka kwa wakulima na itaanza na tani 700 (saw ana kilo 700, 000); hatua inayolenga kuongeza mapato ya wakulima wadogo.

Kampuni hiyo ya kimataifa, pia imejitolea kununua kiasi kikubwa cha uzalishaji wa kahawa, ikilenga hasa kusaidia wakulima wanawake.

“Muafaka huu unahusisha upatikanaji wa angalau magunia 10,000 ya kahawa, jumla ya tani 700. Lengo letu kuu ni kusaidia wakulima wanawake na vyama vya ushirika, kwa kutambua mchango wao wa thamani katika sekta ya kahawa,” Bw Gachagua alisema.

 

  • Tags

You can share this post!

Ole wako endapo ulikuwa unamezea mate Mulamwah, amefanya...

ODM yaanza kuzima nyota ya UDA ngome yake Nyanza

T L