• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 4:50 PM
Michael Olunga, Almoez Ali na Philippe Coutinho tegemeo kuokoa Al Duhail

Michael Olunga, Almoez Ali na Philippe Coutinho tegemeo kuokoa Al Duhail

NA GEOFFREY ANENE

MKENYA Michael Olunga, Almoez Ali (Qatar) na Philippe Coutinho (Brazil) Jumanne, Novemba 28, 2023 watategemewa na klabu ya Al Duhail itakayocheza mechi ya kufa-kupona dhidi ya FC Istiklol kutafuta kuokoa kampeni yake kwenye Klabu Bingwa Asia.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Qatar msimu 2022-2023 lazima washinde mechi hiyo yao ya tano katika Kundi E ugani mwao Abdullah Bin Khalifa jijini Doha na kuomba nambari mbili Persepolis ya Iran ipoteze dhidi ya viongozi Al-Nassr kutoka Saudi Arabia ili kuweka hai matumaini ya kusalia mashindanoni.

Kwa sasa, Al-Duhail, ambayo inatiwa makali na kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain Christophe Galtier, inavuta mkia kwa alama moja.

Al Nassr wanaojivunia mastaa kama Cristiano Ronaldo na Sadio Mane, wana pointi 12. Persepolis wamevuna alama saba, Istiklol (mbili) na Al Duhail (pointi moja).

Vijana wa Galtier wataingia uwanjani wakiuguza vichapo viwili mfululizo nyumbani baada ya kupepetwa na Al Rayyan 1-0 katika kipute cha Qatar Stars Cup (Novemba 19) na Al Sadd 1-0 ligini (Novemba 26).

Pia, Al Duhail walilemewa katika michuano yao miwili iliyopita kwenye Klabu Bingwa Asia baada ya kupoteza dhidi ya Persepolis 1-0 (Oktoba 2) na Al-Nassr 3-2 (Novemba 7).

Itakumbukwa Al-Duhail ilifika nusu-fainali ya Klabu Bingwa Asia msimu uliopita ikilimwa 7-0 na Al-Hilal Saudi.

  • Tags

You can share this post!

Mwalimu mkuu wa shule Kiambu ahimiza wazazi kukumbatia CBC...

Raila: Serikali ya Ruto ni ya drama tupu, hata KCPE...

T L