• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Mkate wa shayiri na ndizi

Mkate wa shayiri na ndizi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

IKIWA unapenda kula mkate ambao umeuoka nyumbani, mkate huu wa ndizi wenye afya ndio bora kabisa.

Chini ya muda wa saa moja, utakuwa na kipande cha mkate wa ndizi uliolowa unyevu na mtamu.

Mkate wa ndizi hutengenezwa kwa viambato vinavyofaa na huongezwa utamu wa asili wa asali na ndizi.

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • Shayiri; unaweza kununua hii kwa bei nafuu.
  • Unga wa ngano
  • Poda ya kuoka
  • Hamira
  • Chumvi
  • Mayai
  • Mafuta ya nazi – Hakikisha kuwa imeyeyuka.
  • Syrup ya maple au asali
  • Vanilla
  • Ndizi – kadiri ndizi zinavyoiva, ndivyo mkate utakavyokuwa bora zaidi.
  • Chokoleti – Inafaa kwa kuongeza ladha ya utamu

Maelekezo

Washa ovena hadi joto la sentigredi 180. Paka mafuta kiasi kwenye chombo cha kuokea na ukiweke kando.

Changanya viungo vilivyo kavu kwa pamoja. Viungo hivi ni shayiri, unga wa ngano, hamira, soda ya kuokea na chumvi.

Katika bakuli kubwa, changanya mayai, mafuta ya nazi, asali na vanila.

Ongeza ndizi zilizoiva na uponde kisha chananya kwa nguvu mpaka kila kitu kiwe kimeunganishwa vizuri.

Changanya mchanganyiko wa unga na wa shayiri, kisha ongezea chipsi za chokoleti kwenye unga.

Mimina mchanganyiko kwenye chombo cha kuokea kilichoandaliwa tayari.

Oka kwa dakika 50.

Epua na ufurahie mara mkate utakapokuwa umepoa.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Kitoweo cha nyama ya ng’ombe

Baadhi ya visababishi vya kiungulia

T L