• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Mkenya aanza kutembea kilomita 500 kuchangisha pesa za kujenga uga wa kisasa Kibra

Mkenya aanza kutembea kilomita 500 kuchangisha pesa za kujenga uga wa kisasa Kibra

NA FARHIYA HUSSEIN

MKENYA amejipatia changamoto ya kutembea safari ya kilomita 488 kutoka Mombasa hadi Nairobi kuchangisha pesa za kujenga uwanja wa michezo wa thamani ya Sh66 milioni.

Uwanja huo utafaidi shule ya msingi ya Olympic na jamaa ya mtaa wa Kibra, Nairobi.

Mkuu wa shirika la Restoring Issachar’s Generation (RIG East Africa) Bi Cynthia Nyamai ambaye alianza kutembea rasmi siku ya Ijumaa iliyopita katika bustani ya Mama Ngina Waterfront mjini Mombasa anatarajiwa kuwasili Nairobi Desemba 15.

Mradi huo unatarajiwa kuanza Januari 2024.

Bi Cynthia Nyamai alisema shule hiyo inahitaji uwanja mzuri na akisisitiza kuna changamoto nyingi zinazowakabili watoto kwa kukosa uwanja wa kuchezea.

“Tunalenga kujenga uwanja ambao unaweza kushughulikia shughuli mbalimbali za michezo na uwezekano wa kuandaa matukio kama vile michezo ya AFCON,” Bi Nyamai alisema.

  • Tags

You can share this post!

Waliohusika na sheria dhidi ya ushoga Uganda kunyimwa...

Raila achemkia Serikali kufuatia kukamatwa kwa Msimamizi wa...

T L