• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:55 AM
Mkopo mpya wa Eurobond kuzidi kuumiza wananchi

Mkopo mpya wa Eurobond kuzidi kuumiza wananchi

Na VALENTINE OBARA

HATUA ya serikali kuchukua mkopo mpya wa Eurobond Alhamisi ilisababisha hamaki kwa Wakenya wengi wanaohofia itaendelea kusababisha hali ngumu ya maisha kwa wananchi.

Takwimu za Benki Kuu ya Kenya zinaonyesha kufikia Septemba 2018, Kenya ilikuwa na madeni ya jumla ya Sh5.1 trilioni, ambazo zimekopeshwa kutoka kwa wawekezaji wa humu nchini na mataifa ya kigeni yakiongozwa na Uchina.

Mkopo mpya wa Eurobond wa Sh210 bilioni, ambao ni wa tatu kuchukuliwa tangu Rais Uhuru Kenyatta alipoingia mamlakani mnamo 2013, umesababisha madeni ya taifa hilii kuongezeka zaidi.

Hii inamaanisha sasa ikiwa Wakenya wote karibu milioni 45 watahitajika kuchangia malipo ya mikopo iliyopo, kila mmoja atatakikana kugharamia zaidi ya Sh117,000.

Kulingana na serikali, Sh75 bilioni kutoka kwa fedha hizo zitatumiwa kulipa madeni machache ya awali.

Waziri wa Fedha, Bw Henry Rotich alisema mbali na kutumiwa kulipa baadhi ya madeni yaliyochukuliwa awali, mkopo huo utagharamia miradi kadhaa ya miundomsingi na mahitaji mengine kwenye bajeti ya taifa ambayo imepangiwa kusomwa mwezi ujao.

“Wawekezaji waliridhika kwamba utekelezaji wa ajenda nne kuu za maendelea utasaidia kuongeza kasi ya ustawi wa taifa, kutoa nafasi zaidi za ajira, kuboresha maisha na kuwezesha ugavi sawa wa mali miongoni mwa Wakenya,” akasema Bw Rotich kwenye tangazo alilotoa kuhusu mkopo huo.

Mwaka uliopita, serikali ililazimika kutoza ushuru kwa bidhaa muhimu na huduma zinazotegemewa sana kimaisha kwenye bajeti ya taifa. Hatua hiyo iliaminika kulenga kuongeza mapato ya serikali ili kugharamia madeni mengi yaliyopo.

Kiongozi wa Chama cha Amani National Congress (ANC), Bw Musalia Mudavadi, alionya madeni hayo yatafanya hali ya maisha izidi kuwa ngumu.

You can share this post!

Al-Shabaab wageuza madaktari wa Cuba watumwa wao

Mzee Moi kulipa Sh1 bilioni kwa kunyakua shamba la mjane

adminleo