• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 10:06 AM
Msamaha gerezani: Wakenya wataka utaratibu ubadilike

Msamaha gerezani: Wakenya wataka utaratibu ubadilike

NA KENYA NEWS AGENCY

WAKENYA wanataka wafungwa wanaosemehewa na rais wawe ni wale tu waliorekebishika tabia.

Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa Jopokazi la kurekebisha kifungu cha Katiba kuhusu msamaha kwa wafungwa, Lydia Muriuki, wananchi wengi wanataka wanaosamehewa wapigwe msasa kwanza kuhakikisha wamerekebisha tabia.

Haya yanajiri baada ya mfungwa aliyesamehewa na Rais Uhuru Kenyatta miezi michache iliyopita kumuua mamake .

Bi Muriuki aliongeza kuwa Wakenya wanataka wanaosamehewa kukabidhiwa cheti cha kibali kitakachowawezesha kupata huduma kwenye taasisi zote za serikali.

“Wakazi wa Kaunti ya Trans Nzoia walipendekeza kuwa watakaosamehewa na Rais wakabidhiwe cheti maalum kitakachowapa idhini ya kupokea huduma katika ofisi zote za serikali,” akasema Bi Muriuki.

Hata hivyo, alisema kuwa cheti hicho cha kibali kitachukuliwa ikiwa mfungwa huyo atatenda uhalifu tena.

“Ikiwa mfungwa huyo atatenda uhalifu tena, basi cheti chake kitachukuliwa. Tunataka kuhakikisha kuwa wafungwa wote waliosamehewa wanaendelea na maisha yao kama kawaida,” akaongeza Bi Muriuki.

  • Tags

You can share this post!

Gari la kampeni za Orengo lateketea jenereta ilipolipuka

Ugavana: Wazee wa Kaya wambariki Kithi

T L