• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Mtandao wa ‘Ardhi Sasa’ utaweza kuzima matapeli wa ardhi Nairobi na Kenya kwa jumla?

Mtandao wa ‘Ardhi Sasa’ utaweza kuzima matapeli wa ardhi Nairobi na Kenya kwa jumla?

Na SAMMY WAWERU

MUDA unazidi kuyoyoma tangu ubomoaji wa majengo ufanyike katika eneo la Kware, Kaunti Ndogo ya Njiru, kiungani mwa jiji la Nairobi.

Matumaini ya wahasiriwa kupata haki, yanaendelea kufifia serikali ikisalia kimya, huku wakihangaika kusukuma gurudumu la maisha.Waathiriwa walikuwa wakazi waliojiweza, ila sasa wengi wao hawana uwezo.Zaidi ya watu 5, 000 waliachwa bila makao, kufuatia ubomozi huo ulioanza usiku wa kuamkia Machi 26, 2021.

Ulitekelezwa kwa muda wa siku kadhaa, chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya pamoja vya usalama.Kulingana na Jacinta Wanjiku Macharia, ambaye ni mke na mama wa mtoto mmoja, zoezi la kuangusha majengo lilianza mwendo wa saa tisa alfajiri.

“Tuliamshwa na gesi ya vitoa machozi iliyorushwa na maafisa wa usalama saa tisa alfajiri, tukitakiwa kuondoka mara moja,” Jecinta anadokeza.Nyumba yake ilikuwa kati ya zilizotanguliwa.Hakuna alichoweza kunusuru, ila mavazi waliyokuwa nayo mwilini. Anachoshukuru Mungu ni kuokoa mwanawe mwenye umri wa miaka mitatu.

Jacinta ni mjamzito na anatarajia kujifungua wakati wowote kuanzia sasa.Anasema, mahandaki yalichimbwa, katika kile kilionekana kama kuzuia wakazi walioathirika kusafirisha vifaa na mali ambayo wangeweza kuokoa.Chini ya dakika na saa chache, makazi yake yakafanywa vipande vya saruji, changarawe na mawe yasiyo na maana.

“Polisi waliotumwa hawakuturuhusu tuokoe chochote,” anasema, akiongeza kwamba kilichomuuma zaidi ni afisa mmoja kumueleza “amri ilitoka juu”.Mhasiriwa mwingine ni Eunice Wachira. “Makao yangu yaliangushwa siku ya pili, Machi 27, 2021. Ubomozi ulipoanza, nilidhani walilenga nyumba zilizokuwa karibu na mto,” anaelezea.

Picha/ Sammy Waweru.
Jacinta Wanjiku Machira akiwa ilipokuwa ploti yake eneo la Kware, Njiru, Nairobi.

Kwa mujibu wa masimulizi ya mama huyu wa watoto wawili, siku ya tukio alikuwa amepeleka mvulana wake mdogo kliniki katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH).

“Tuliporejea, tulipata maafisa chungu nzima wa polisi wakishika doria na kufurusha watu. Mali yangu yalipotelea humo, sikuweza kuingia,” Eunice anafichua, akisema baadaye alirejea na kuokoa tangi la maji pekee.

Naye Michael Mwangi, mwathiriwa mwingine anakadiria hasara ya mali yenye thamani ya Sh4 milioni.“Kando na nyumba yangu kubomolewa, nilikuwa na duka la vifaa vya ujenzi, ambalo sasa ni historia. Ninahisi uchungu nikikumbuka jasho langu lilivyoangushwa chini ya saa chache,” Mwangi analia.

Huku Mwangi akitegemea vibarua vya hapa na pale, anashangaa atakavyoweza kuinuka afike kimaendeleo alipokuwa.

Maelezo ya watatu hao yakiashiria walinunua vipande vyao vya ardhi ipatayo miaka mitatu iliyopita, imebainika eneo la Kware limekuwa na mzozo wa umiliki kwa zaidi ya miaka 20.Kampuni ya Njiru Ageria imetajwa kuwa mmiliki.

Wahasiriwa wanahoji vyeti walivyokabidhiwa baada ya ununuzi vinaonyesha ardhi hiyo ni mradi wa maskwota, unaomilikiwa na Investors Settlement Field.“Ni muhimu kabla ya kununua ardhi upitie afisi ya serikali iliyoko karibu, kama vile chifu, ili kupata historia ya eneo unalonuwia kununua ploti au shamba kuwekeza.

“Hilo litasaidia kujua uhalisia wa umiliki na endapo ardhi unayolenga ina mzozo,” akashauri afisa mmoja wa utumishi wa umma Kware, na aliyeomba kubana majina yake kwa sababu haruhusiwi kuzungumza na wanahabari.

Jacinta Wanjiku na Eunice Wachira wanaiambia Taifa Leo Dijitali kwamba walinunua vipande vyao vya ploti mwaka wa 2018.“Kwa ushirikiano na mume wangu ambaye huchuuza malimali kwa wilibaro tulijinyima tukanunua ploti ambayo sasa haipo, kima cha Sh330, 000 na kuiboresha kwa zaidi ya Sh400, 000 kuwa makao,” Wanjiku anadokeza.

Ardhi ya Wanjiku ilikuwa yenye ukubwa wa mita 30 kwa 60. Eunice anasema wakati wa kununua kipande chao, mume wake alikuwa dereva wa matrela ya masafa marefu.Aidha, walikinunua Sh280, 000, na ambacho kina ukubwa wa mita 30 kwa 60 pia. “Tulichukua mkopo wa Sh800, 000 kufanya ujenzi wa makao ambayo sasa ni mahame,” Eunice anaelezea.

Huku umiliki eneo lililoathirika ukisalia kitendawili kilichokosa mteguzi, chifu wa kata ya Njiru, Teresia Wambui kwenye mahojiano ya kipekee alisema ardhi hiyo ni ya kibinafsi, na haihusishwi na serikali.“Siku ya tukio nilipigiwa simu mwendo wa saa kumi alfajiri. Sikuwa nimearifiwa chochote na ubomoaji ulinifikia kwa mshangao,” Wambui akasema.

Idara ya usalama eneo hilo nayo haikuwa radhi kueleza ikiwa ardhi hiyo yenye utata ni mali ya unyakuzi au la.“Ilikuwa oparesheni ya vikosi vya pamoja, na hilo linapojiri halina jawabu,” akasema Paul Wambugu OCPD Kayole, akikwepa kueleza iwapo kulikuwa na amri ya korti.

Ni bomoabomoa ambayo wahasiriwa wameendelea kusalia na maswali chungu nzima, kwa nini shughuli ya aina hiyo itekelezwe kipindi ambacho janga la Covid-19 linaendelea kusaga uchumi.

Isitoshe, ubomozi ulifanyika siku ambayo Rais Uhuru Kenyatta alitangaza amri ya ama kuingia au kutoka kaunti tano, ikiwemo Nairobi, zilizotajwa kuwa hatari katika maambukizi ya virusi vya corona.Amri hiyo hata hivyo iliondolewa mwezi mmoja baadaye.Walioathirika wasingeweza kusafiri mashambani, wanakotoka ili kuendelea kusukuma gurudumu la maisha.

“Endapo ilikuwa ardhi ya unyakuzi kama wanavyodai, kwa nini wasingetueleza mapema tuondoe mali yetu badala ya uharibifu wa aina hiyo? Kilikuwa kitendo cha ukatili na kukosa utu,” Jacinta Wanjiku anasema, akielezea kushangazwa kwake.

Ubomozi wa eneo la Kware si wa kwanza kushuhudiwa katika Kaunti ya Nairobi.Eneo la Ruai, Embakasi, Kariobangi na Zimmerman, yameshuhudia ubomoaji sawa na huo.Ni bomoabomoa ya makao ya Wakenya waliojinyima mengi ili kuwekeza, inayoibua maswali mazito kuhusu uhalisia wa umiliki wa ardhi Nairobi na pia maeneo mengine nchini ambayo hushuhudia taswira kama hiyo.

Visa vya unyakuzi wa ardhi ya kibinafsi na pia umma zipo na hushuhudiwa mara kwa mara maeneo tofauti nchini, ila hili suala la Nairobi linazidi kuibua maswali ikiwa ni njama, mchakato na mtandao wa utapeli unaosakatwa.

Umewadia wakati Wizara ya Ardhi na taasisi husika ziwajibike ili kuokoa Wakenya wasio na hatia wanaponunua ploti au mashamba.Sidhani ikiwa kuna mtu mwenye akili razini anaweza kuhatarisha raslimali zake katika mpango wenye utata, hasa masuala ya ardhi.

Yote tisa, kumi mpango wa utoaji huduma za mashamba kwa njia ya kidijitali uliozinduliwa Aprili 27, 2021 na Rais Uhuru Kenyatta unasubiriwa kuona iwapo utasaidia kuangazia kero ya utapeli na unyakuzi wa ardhi nchini.

“Leo imekuwa siku ya historia Kenya kupiga hatua mbele, kupitia uzinduzi wa mtandao wa kitaifa kusaidia katika utoaji wa huduma za ardhi,” akasema Rais Kenyatta wakati wa uzinduzi wa mpango huo.Aidha, mtandao huo maarufu kama ‘Ardhi Sasa’ umetajwa kuwa utawezesha wanunuzi kupiga msasa uhalisia wa ardhi wanayolenga.

Kulingana na kiongozi wa nchi, teknolojia hiyo ya kidijitali vilevile itasaidia kuondoa mtandao wa matapeli wa mashamba Kenya.“Wakenya wengi wameteseka sana kwa kununua mashamba ambayo hayapo, hewa, mashamba ambayo yameuziwa mtu mwingine na mengine hatimiliki kubadilishwa na matapeli.

MUDA unazidi kuyoyoma tangu ubomoaji wa majengo ufanyike katika eneo la Kware, Kaunti Ndogo ya Njiru, kiungani mwa jiji la Nairobi.Matumaini ya wahasiriwa kupata haki, yanaendelea kufifia serikali ikisalia kimya, huku wakihangaika kusukuma gurudumu la maisha.

Waathiriwa walikuwa wakazi waliojiweza, ila sasa wengi wao hawana uwezo.Zaidi ya watu 5, 000 waliachwa bila makao, kufuatia ubomozi huo ulioanza usiku wa kuamkia Machi 26, 2021.Ulitekelezwa kwa muda wa siku kadhaa, chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya pamoja vya usalama.

Kulingana na Jacinta Wanjiku Macharia, ambaye ni mke na mama wa mtoto mmoja, zoezi la kuangusha majengo lilianza mwendo wa saa tisa alfajiri.“Tuliamshwa na gesi ya vitoa machozi iliyorushwa na maafisa wa usalama saa tisa alfajiri, tukitakiwa kuondoka mara moja,” Jecinta anadokeza.

Nyumba yake ilikuwa kati ya zilizotanguliwa.Hakuna alichoweza kunusuru, ila mavazi waliyokuwa nayo mwilini. Anachoshukuru Mungu ni kuokoa mwanawe mwenye umri wa miaka mitatu.Jacinta ni mjamzito na anatarajia kujifungua wakati wowote kuanzia sasa.

Anasema, mahandaki yalichimbwa, katika kile kilionekana kama kuzuia wakazi walioathirika kusafirisha vifaa na mali ambayo wangeweza kuokoa.Chini ya dakika na saa chache, makazi yake yakafanywa vipande vya saruji, changarawe na mawe yasiyo na maana.

“Polisi waliotumwa hawakuturuhusu tuokoe chochote,” anasema, akiongeza kwamba kilichomuuma zaidi ni afisa mmoja kumueleza “amri ilitoka juu”.Mhasiriwa mwingine ni Eunice Wachira. “Makao yangu yaliangushwa siku ya pili, Machi 27, 2021. Ubomozi ulipoanza, nilidhani walilenga nyumba zilizokuwa karibu na mto,” anaelezea.

Kwa mujibu wa masimulizi ya mama huyu wa watoto wawili, siku ya tukio alikuwa amepeleka mvulana wake mdogo kliniki katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH).“Tuliporejea, tulipata maafisa chungu nzima wa polisi wakishika doria na kufurusha watu. Mali yangu yalipotelea humo, sikuweza kuingia,” Eunice anafichua, akisema baadaye alirejea na kuokoa tangi la maji pekee.

Naye Michael Mwangi, mwathiriwa mwingine anakadiria hasara ya mali yenye thamani ya Sh4 milioni.“Kando na nyumba yangu kubomolewa, nilikuwa na duka la vifaa vya ujenzi, ambalo sasa ni historia. Ninahisi uchungu nikikumbuka jasho langu lilivyoangushwa chini ya saa chache,” Mwangi analia.

Huku Mwangi akitegemea vibarua vya hapa na pale, anashangaa atakavyoweza kuinuka afike kimaendeleo alipokuwa.Maelezo ya watatu hao yakiashiria walinunua vipande vyao vya ardhi ipatayo miaka mitatu iliyopita, imebainika eneo la Kware limekuwa na mzozo wa umiliki kwa zaidi ya miaka 20.

Kampuni ya Njiru Ageria imetajwa kuwa mmiliki.Wahasiriwa wanahoji vyeti walivyokabidhiwa baada ya ununuzi vinaonyesha ardhi hiyo ni mradi wa maskwota, unaomilikiwa na Investors Settlement Field.“Ni muhimu kabla ya kununua ardhi upitie afisi ya serikali iliyoko karibu, kama vile chifu, ili kupata historia ya eneo unalonuwia kununua ploti au shamba kuwekeza.

“Hilo litasaidia kujua uhalisia wa umiliki na endapo ardhi unayolenga ina mzozo,” akashauri afisa mmoja wa utumishi wa umma Kware, na aliyeomba kubana majina yake kwa sababu haruhusiwi kuzungumza na wanahabari.

Jacinta Wanjiku na Eunice Wachira wanaiambia Taifa Leo Dijitali kwamba walinunua vipande vyao vya ploti mwaka wa 2018.“Kwa ushirikiano na mume wangu ambaye huchuuza malimali kwa wilibaro tulijinyima tukanunua ploti ambayo sasa haipo, kima cha Sh330, 000 na kuiboresha kwa zaidi ya Sh400, 000 kuwa makao,” Wanjiku anadokeza.

Ardhi ya Wanjiku ilikuwa yenye ukubwa wa mita 30 kwa 60.Eunice anasema wakati wa kununua kipande chao, mume wake alikuwa dereva wa matrela ya masafa marefu.Aidha, walikinunua Sh280, 000, na ambacho kina ukubwa wa mita 30 kwa 60 pia. “Tulichukua mkopo wa Sh800, 000 kufanya ujenzi wa makao ambayo sasa ni mahame,” Eunice anaelezea.

Huku umiliki eneo lililoathirika ukisalia kitendawili kilichokosa mteguzi, chifu wa kata ya Njiru, Teresia Wambui kwenye mahojiano ya kipekee alisema ardhi hiyo ni ya kibinafsi, na haihusishwi na serikali.“Siku ya tukio nilipigiwa simu mwendo wa saa kumi alfajiri. Sikuwa nimearifiwa chochote na ubomoaji ulinifikia kwa mshangao,” Wambui akasema.

Idara ya usalama eneo hilo nayo haikuwa radhi kueleza ikiwa ardhi hiyo yenye utata ni mali ya unyakuzi au la.“Ilikuwa oparesheni ya vikosi vya pamoja, na hilo linapojiri halina jawabu,” akasema Paul Wambugu OCPD Kayole, akikwepa kueleza iwapo kulikuwa na amri ya korti.

Ni bomoabomoa ambayo wahasiriwa wameendelea kusalia na maswali chungu nzima, kwa nini shughuli ya aina hiyo itekelezwe kipindi ambacho janga la Covid-19 linaendelea kusaga uchumi.Isitoshe, ubomozi ulifanyika siku ambayo Rais Uhuru Kenyatta alitangaza amri ya ama kuingia au kutoka kaunti tano, ikiwemo Nairobi, zilizotajwa kuwa hatari katika maambukizi ya virusi vya corona.

Amri hiyo hata hivyo iliondolewa mwezi mmoja baadaye.Walioathirika wasingeweza kusafiri mashambani, wanakotoka ili kuendelea kusukuma gurudumu la maisha.“Endapo ilikuwa ardhi ya unyakuzi kama wanavyodai, kwa nini wasingetueleza mapema tuondoe mali yetu badala ya uharibifu wa aina hiyo? Kilikuwa kitendo cha ukatili na kukosa utu,” Jacinta Wanjiku anasema, akielezea kushangazwa kwake.

Ubomozi wa eneo la Kware si wa kwanza kushuhudiwa katika Kaunti ya Nairobi.Eneo la Ruai, Embakasi, Kariobangi na Zimmerman, yameshuhudia ubomoaji sawa na huo.Ni bomoabomoa ya makao ya Wakenya waliojinyima mengi ili kuwekeza, inayoibua maswali mazito kuhusu uhalisia wa umiliki wa ardhi Nairobi na pia maeneo mengine nchini ambayo hushuhudia taswira kama hiyo.

Visa vya unyakuzi wa ardhi ya kibinafsi na pia umma zipo na hushuhudiwa mara kwa mara maeneo tofauti nchini, ila hili suala la Nairobi linazidi kuibua maswali ikiwa ni njama, mchakato na mtandao wa utapeli unaosakatwa.

Umewadia wakati Wizara ya Ardhi na taasisi husika ziwajibike ili kuokoa Wakenya wasio na hatia wanaponunua ploti au mashamba.Sidhani ikiwa kuna mtu mwenye akili razini anaweza kuhatarisha raslimali zake katika mpango wenye utata, hasa masuala ya ardhi.

Yote tisa, kumi mpango wa utoaji huduma za mashamba kwa njia ya kidijitali uliozinduliwa Aprili 27, 2021 na Rais Uhuru Kenyatta unasubiriwa kuona iwapo utasaidia kuangazia kero ya utapeli na unyakuzi wa ardhi nchini.

“Leo imekuwa siku ya historia Kenya kupiga hatua mbele, kupitia uzinduzi wa mtandao wa kitaifa kusaidia katika utoaji wa huduma za ardhi,” akasema Rais Kenyatta wakati wa uzinduzi wa mpango huo.Aidha, mtandao huo maarufu kama ‘Ardhi Sasa’ umetajwa kuwa utawezesha wanunuzi kupiga msasa uhalisia wa ardhi wanayolenga.

Kulingana na kiongozi wa nchi, teknolojia hiyo ya kidijitali vilevile itasaidia kuondoa mtandao wa matapeli wa mashamba Kenya.“Wakenya wengi wameteseka sana kwa kununua mashamba ambayo hayapo, hewa, mashamba ambayo yameuziwa mtu mwingine na mengine hatimiliki kubadilishwa na matapeli.

“Hatua tuliyopiga leo (kuzindua mtandao wa Ardhi Sasa) itasaidia wanunuzi kupata hatimiliki halali,” akasema Rais Kenyatta, akiongeza kuwa uzinduzi huo ndio njia pekee kuondoa maovu ya ardhi ambayo yamekuwa yakishuhudiwa.

Wanjiku akisimulia ubomoaji ulivyotekelezwa katika eneo la Kware, kuanzia asubuhi ya kuamkia Machi 26, 2021.
  • Tags

You can share this post!

Kenya imechanja tena wanamichezo 2,000 na wanaotangamana...

Tungali kwenye mataa baada ya kubomolewa makao