• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Mto Ewaso Nyiro waendelea kukauka athari hasi za mabadiliko ya tabianchi zikionekana wazi

Mto Ewaso Nyiro waendelea kukauka athari hasi za mabadiliko ya tabianchi zikionekana wazi

NA SAMMY WAWERU

SAMBURU ni miongoni mwa kaunti zilizoorodheshwa kusakamwa na janga la ukame. 

Kwa zaidi ya miaka mitatu mfululizo, kaunti zisizopungua 24 zimeathirika kutokana na kiangazi cha muda mrefu.

Hali hiyo imetajwa kuchangiwa na tabianchi, Upembe wa Afrika ukiathirika kwa kiwango kikubwa.

Nchi zilizolemewa na ukame zinajumuisha Kenya, Somalia na Ethiopia.

Kaunti ya Samburu inafahamika kwa shughuli ya ufugaji, kupitia jamii za kuhamahama.

Tegemeo kuu lao la maji likiwa Mto Ewaso Nyiro, ukame unaoendelea umesababisha kiwango cha maji kupungua kwa kasi yaliyosalia yakitajwa kuwa “kiduchu”.

“Yanayotiririka ni haba mno,” mmoja wa wakazi akaambia Taifa Leo wakati wa mahojiano eneo la Maralal, akiomba kubana jina lake.

Ni hali inayochochea wanyamapori kama vile ndovu, kuvamia makazi ya binadamu.

Kulingana na afisa wa hifadhi moja ya wanyamapori eneo hilo, wenyeji wanane wamepoteza maisha kufuatia “mzozano kati ya wanyama – ndovu na binadamu”.

Idadi kubwa ya wakazi, wanajushughulisha na ufugaji wa ng’ombe na kondoo.

Vilevile, kuna wanaoendeleza ufugaji wa ngamia ili kuwasaidia kusafirisha maji.

Baadhi ya maeneo kame, mifugo wameripotiwa kufa njaa wenyeji malisho na mimea ikikauka.

Wenyeji maeneo iliyosakamwa na ukame wanategemea chakula cha msaada kinachosambazwa na serikali, kwa ushirikiano na wasamaria wema.

  • Tags

You can share this post!

Uvumbuzi: Trekta inayotumika kwenye mashamba madogo

Liverpool wamaliza kampeni za Kundi A kwenye UEFA katika...

T L