• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 1:29 PM
Mumias: Bwanyenye Jaswant Rai aamua kuondoa kesi

Mumias: Bwanyenye Jaswant Rai aamua kuondoa kesi

NA SAM KIPLAGAT

BWANYENYE Jaswant Singh Rai ameondoa kesi zote zilizokwama mahakamani ambazo zimekuwa kikwazo kwa juhudi za kufufua kiwanda cha sukari cha Mumias.

Bwanyenye huyo, kupitia kwa kampuni yake ya West Kenya, alikuwa amepinga kandarasi ya nduguye na mshindani wake kibiashara Sarbjit Singh Rai kuchukua mikoba ya udhibiti wa kiwanda hicho.

Kampuni ya Sarrai Group ilipata kandarasi ya miaka 20 kuendeleza shughuli za kufufua kiwanda hicho.

West Kenya sasa imewasilisha notisi tatu za kuonyesha nia ya kuondoa kesi mbele ya Mahakama ya Rufaa.

Rufaa hizo, ambazo hazijasikilizwa, zilikuwa zimewasilishwa na benki ya KCB na mrasimu PVR Rao, baada ya Mahakama Kuu kuagiza mrasimu aondoke. Jaji Alfred Mabeya alitoa uamuzi huo mnamo Aprili 2022.

Rufaa ya pili iliwasilishwa na Sarrai Group, huku kesi ya tatu ikiwa ni rufaa dhidi ya mashtaka ya kukiuka maagizo ya mahakama dhidi ya Sarbjit, Rakesh Kumar na Stephen Kihumba, waliopatikana na hatia ya kupuuza agizo la mahakama kwamba wasitishe shughuli zao katika kiwanda cha Mumias.

Hatua ya Jaswant Rai inajiri siku chache baada ya Rais William Ruto kuwaonya vikali wanaotatiza shughuli za kufufua viwanda vya sukari nchini akiwaambia “mambo ni matatu”.

  • Tags

You can share this post!

Namuomba Mungu wa mwisho awe ni wewe – Hamisa Mobetto

Watu 70 wafariki kwenye mkasa wa moto Johannesburg

T L