• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 5:20 PM
Mwanasheria mkuu kukata rufaa kuhusu uteuzi wa majaji

Mwanasheria mkuu kukata rufaa kuhusu uteuzi wa majaji

Na JOSEPH WANGUI

MWANASHERIA Mkuu Paul Kihara Kariuki amewasilisha notisi ya kukata rufaa kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu, ambapo Rais Uhuru Kenyatta, aliamrishwa awateue majaji sita aliowakataa hapo awali ndani ya siku 14 zijazo.

Bw Kariuki alisema hajaridhishwa na uamuzi huo uliotolewa na majaji George Dulu, William Musyoka na James Wakiaga, mnamo Alhamisi wiki jana.

Kupitia Naibu Wakili Mkuu wa serikali Emmanuel Bitta, Bw Kariuki alisema hajaridhishwa na uamuzi huo uliosema Rais Kenyatta anaweza kupuuzwa katika mchakato wa kuwateua majaji wapya.Majaji ambao Rais Kenyatta alikataa kuwateua ni Mabw George Odunga, Aggrey Muchelule, Joel Ngugi, Weldon Koriri, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Mombasa, Evans Makori pamoja na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Bi Judith Omange.

“Baada ya kukamilika kwa siku 14 bila Rais Kenyatta kufanya uteuzi wa majaji hao, itafasiriwa kuwa hana mamlaka tena kwenye suala hilo na majaji hao watakuwa radhi kuchukua majukumu yao mapya,” uamuzi wa Mahakama Kuu ulisema.

 

You can share this post!

Beki wa zamani wa Man-Utd, Patrice Evra, afichua aliwahi...

Wazee wakemea viongozi kunyamazia mzozo kuhusu bahari

T L