• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 5:54 PM
Mwanasiasa adai kutekwa na kutupwa msituni

Mwanasiasa adai kutekwa na kutupwa msituni

Na Titus Ominde

MWANASIASA wa Kiambu aliyesemekana kutekwa nyara na watu waliojidai kuwa maafisa wa polisi mnamo Jumatano alasiri, jana asubuhi alijikuta katika msitu wa Sengalo katika Kaunti ndogo ya Kesess.

John Njuguna, ambaye ni mshirika wa karibu wa Naibu wa Rais William Ruto, alidai kwamba watekaji nyara ambao walikuwa na silaha walimlazimisha kuingia kwenye gari la kibinafsi wakiitshia kumpiga risasi iwapo angekosa kushirikiana nao.

Bw Njuguna alisema watu hao watatu wenye silaha walimsafirisha kutoka Nairobi kuelekea Nakuru huku wakimtishia kumuua ikiwa hataachana na azma yake ya kugombea kiti cha ubunge cha Kiambaa.

Vile vile alidai kuporwa Sh180,000 pesa taslimu, kompyuta ndogo na mkoba wake uliokuwa na vyeti vyake.

Mwanasiasa huyo alisema watekaji nyara wake walikuwa wamefunika macho yake kwa kutumia kipande cha njia hadi msitu wa Sengalo.Alisema kuwa watekaji walimpiga makofi kadhaa baada ya kumvua nguo mwishowe walimfunga mikono kwa mti msituni humo ambapo walimwacha mwendo wa saa tisa usiku.

‘Walinipiga kofi na kunivua nguo kabla ya kunifunga mikono juu ya mti msituni,’ akasema Bw Njuguna. Aliongeza kuwa baada ya kujinasua kutoka kwenye mti alijikokota hadi barabara kuu ya Kapsebet-Nakuru ambapo alipata mekaniki wakitengeneza gari ambao walimsaidia kwa nguo.

Hatimaye mafundi hao wlaimsaidia kupata lifti hadi mjini Elodret ambapo aliripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Eldoret.

  • Tags

You can share this post!

Olunga nje ya Kombe la Dunia la Klabu

Raila asema anaweza kuingia handisheki na Ruto