• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Nairobi City Stars wasajili beki matata raia wa Uganda

Nairobi City Stars wasajili beki matata raia wa Uganda

Na CHRIS ADUNGO

NAIROBI City Stars wamemsajili nyota wa timu ya taifa ya Uganda, Yusuf Lubowa Mukisa kutoka Proline FC.

Mukisa anaingia katika sajili rasmi ya City Stars almaarufu Simba wa Nairobi kwa mkataba wa miaka miwili. Anatarajiwa sasa kujaza nafasi ya beki wa kulia Kevin Okumu ambaye tayari ameyoyomea kambini mwa Wazito FC.

“Uji wa Mukisa utaimarisha zaidi uthabiti wa safu yetu ya ulinzi. Ni mwanasoka wa haiba kubwa ambaye amekuwa tegemeo la Proline FC kwa kipindi kirefu,” akasema mratibu wa kikosi cha City Stars, Samsom Otieno.

Mukisa ni nahodha wa zamani wa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 nchini Uganda.

Amewahi pia kuvalia jezi za miamba wa Ligi Kuu ya Uganda, SC Villa.

Aliwaongoza Vipers kunyanyua ufalme wa Ligi Kuu ya Uganda mnamo 2015-16.

Mukisa alikuwa sehemu ya kikosi kilichotegemewa na Proline katika gozi la Cecafa na CAF Confederations Cup mnamo 2019.

“Nina fahari kujiunga na familia pana ya City Stars wna nilikuja Kenya mnamo Januari 2020 na kuanza kushiriki mazoezi ya pamoja na kikosi hiki kabla ya kuja kwa janga la corona,” akasema Mukisa, 27.

City Stars inafahamika pakubwa kwa kuwa ngome yanaomilikiwa na Wakfu wa Jackson Foundation.

Tumekuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara katika kipindi cha miezi sita iliyopita na kujivunia huduma za wanasoka raia wa Uganda wakiwemo Dan Sserunkuma, Bruno Sserunkuma na Jimmy Bageya miongoni mwa wengine.

Mukisa anakuwa mwanasoka wa tatu wa haiba kubwa kuingia katika sajili rasmi ya City Stars baada ya Erick Ombija kutoka Gor Mahia ba kiungo mkabaji Sven Yidah wa Kariobangi Sharks.

Watatu hao wanaungana na chipukizi wengine waliosajiliwa na City Stars hivi majuzi wakiwemo Rowland Makati (Vapor Sports), Timothy Ouma (Laiser Hill Academy), Ronney Kola Oyaro (Kenya School of Government) na kipa Elvis Ochieng Ochoro aliyesajiliwa kutoka Hakati Sportiff.

You can share this post!

Sita wajiondoa kwenye uchaguzi wa FKF

AWINO: Konokono Mwea wasipuuzwe kama gugumaji Victoria