• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 2:08 PM
Najib Balala alaumiwa kwa kuangusha hoteli za kifahari Nyeri

Najib Balala alaumiwa kwa kuangusha hoteli za kifahari Nyeri

NA MWANGI MUIRURIĀ 

MFANYABIASHARA na mwanasiasa Thuo Mathenge amemlaumu aliyekuwa Waziri wa Utalii katika serikali ya Uhuru Kenyatta kwa kusambaratika kwa biashara za hoteli kubwa Mlima Kenya.

Alisema hoteli za kifahari katika eneo la Mlima Kenya zikiwemo Treetops, Outspan, Green Hills na White Rhino zilifungwa kutokana na Waziri huyo kukandamiza biashara za burudani eneo hilo.

“Kuna vitita ambavyo hutengewa biashara za hoteli. Lakini Bw Balala alitunyima fedha hizo. Ukiambatanisha na janga la Korona, tukajipata hoi,” akasema.

Bw Mathenge ambaye kwa jina maarufu anaitwa Wanguku na aliyewania ugavana Nyeri 2022 lakini akashindwa na Mutahi Kahiga, alisema serikali ya Rais William Ruto inapaswa kuangalia suala hilo.

“Naibu wa Rais Bw Rigathi Gachagua anafaa kutathmini suala hili kwa kina. Tulikandamizwa na Balala na ni wakati wa kurekebisha hali,” akasema.

Akiongea katika kituo cha Inooro, alisema watalii waliokuwa wakitembelea vivutio vya Kaunti ya Nyeri na viunga vyake, walikuwa wakipeleka uteja katika biashara za eneo hilo.

“Lakini tumevunjavunjwa kwa sasa na tuko hoi. Rais Uhuru Kenyatta alimpa kazi Waziri wa kutumaliza. Hoteli zetu zikaanza kuchukuliwa na wengine ambao wanazinunua kwa fujo kwa kuwa sisi tumeishiwa na hela,” akasema.

Bw Mathenge alisema kwamba kwa sasa biashara za hoteli zinachukuliwa na wageni kutoka mataifa ya kigeni.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Ahadi feki za Ruto kuhusu mahindiĀ 

Raila: Ruto amerejesha Kenya kwa utawala wa kidikteta

T L