• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Nyali wahamasishwa kuhusu Covid-19

Nyali wahamasishwa kuhusu Covid-19

Na MISHI GONGO

KUFUATIA ongezeko la maambukizi ya Covid-19 katika Kaunti ya Mombasa katika kile kinatajwa kuchangiwa na wakazi kukiuka masharti ya kudhibiti ugonjwa huo, polisi wamewahamasisha wakazi katika eneo la Nyali kuhusiana na ugonjwa huo.

Shughuli hiyo imefanyika katika mitaa ya mabanda katika eneo hilo, ikiwemo Kisumu Ndogo, Kambi Kikuyu, Kangi na Shauri Yako.

Iliongozwa na koplo wa polisi kituo cha Nyali Bw Anthony Njagi na ilililenga kuhakikisha wakazi wanajua jinsi ya kujilinda wasipate maambukizi na vilevile kuelewa majukumu ya polisi kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo pamoja na kuwakabidhi wakazi barakoa.

Bw Njagi alisema tangu virusi vya corona vianze kuyumbisha dunia, wakazi wa Nyali wamekuwa wakifanya mchezo wa paka na panya na maafisa wa polisi katika utekelezaji wa masharti yaliyowekwa.

“Shughuli hii ni kuwaambiwa wakazi kuwa wanaweza kutii masharti bila ya usimamizi wa maafisa wa polisi,” akasema afisa huyo.

Alisema shughuli hiyo ni muhimu kuhakikisha kuwa wakazi katika mitaa ya mabanda wanajilinda afya zao.

Afisa mkuu wa shirika la vijana la Tabasamu Bi Vivian Jackton aliyeshiriki katika shughuli hiyo, alisema wameungana kutekeleza kwa sababi wakazi wanaoishi katika mitaa ya mabanda wako katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

Alisema ni vigumu kutekeleza sheria ya kutokongamana kufuatia msongamano mkubwa wa watu katika mitaa ya mabanda hivyo inailazimu serikali kuja na njia mbadala za wakazi wa maeneo hayo kujikinga.

You can share this post!

Polisi wampiga risasi babake seneta wa Lamu kwa kutovaa...

Mvurya abainisha mpango wake Kwale kukabili Covid-19

adminleo