• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Nyota 5 kuwakilisha Kenya kwenye Mashindano ya Dunia ya Chesi nchini Ujerumani

Nyota 5 kuwakilisha Kenya kwenye Mashindano ya Dunia ya Chesi nchini Ujerumani

NA TOTO AREGE

WACHEZAJI watano wa timu ya wanabenki wa KCB ya Sataranji yaani chesi, wanatarajiwa kuondoka nchini mnamo Jumatano kuelekea Dusseldorf, Ujerumani kwa Mashindano ya Dunia kuanzia Agosti 25 hadi 29.

Wachezaji hao watano ni Ben Nguku, Martin Njoroge, Joyce Nyaruai, Joseph Methu na Robert Mcligeyo.

Wataongozwa na mchezaji mkongwe wa Chess ambaye pia ni kocha Ben Magana.

Watano hao pia wameiwakilisha nchi katika Olympiad ya Dunia ya Chess. Methu na Mcligeyo walikuwa vinara wa zamani, Njoroge ndiye mshindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Chess ya 2021 (KNCC).

Wanabenki hao watakuwa wawakilishi pekee wa Kenya katika shindano hilo, kutokana na matokeo mazuri katika mashindano ya Ligi Kuu ya Kenya ya Chess mwaka 2022.

Mashindano hayo ya kila mwaka huleta pamoja klabu kutoka kote ulimwenguni na itakuwa mara ya kwanza kwa timu ya Kenya kushiriki.

Nyaruai ni bingwa wa KNCC upande wa wanawake. Kulingana na Meneja wa Timu ya KCB Isaac Babu, mabingwa hao wamekuwa wakijiandaa tangu Machi.

Kocha Msaidizi Philip Singe amekuwa akimsaidia Magana katika kuwaandaa wachezaji kwa ajili ya michuano hiyo.

“Tumefanya mazoezi vizuri. Tunashukuru KCB kwa msaada ambao benki imeipa timu. Tutajitahidi kuwakilisha nchi vyema,” alisema Babu.

  • Tags

You can share this post!

Wakazi wa vijiji vilivyoshambuliwa Lamu watafuta maeneo...

Mshukiwa wa mauaji ya afisa wa DCI naye auawa kwa risasi

T L