• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Obama akashifu Hamas kwa ‘shambulizi la kigaidi lenye ujasiri bila aibu’ dhidi ya Israel

Obama akashifu Hamas kwa ‘shambulizi la kigaidi lenye ujasiri bila aibu’ dhidi ya Israel

NA LABAAN SHABAAN

ALIYEKUWA  Rais wa Amerika, Barack Obama, amevunja kimya chake kuhusu mashambulizi kati ya Israel na Palestina.

Bw Obama alikemea vikali shambulizi la Hamas dhidi ya Israel akisema ni  ‘uvamizi wa kigaidi wenye ujasiri bila aibu.’

Katika taarifa yake iliyosubiriwa sana kwa jinsi alivyo na ufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Bw Obama ameunga mkono Israel kukabili Hamas.

Kwa moto uo huo, rais wa 44 wa Amerika ametoa wito wa  mchakato wa maridhiano ili kuleta amani ya kudumu kati ya Israel na Palestina.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X (awali Twitter), Bw Obama alisema, “Waamerika wote wanafaa kutishwa na kukasirishwa na uvamizi wa kigaidi wenye ujasiri bila aibu Israel na kuchinjwa kwa raia wasio na hatia.”

“Tunaomboleza waliofariki, kuombea waliotekwa nyara warejee salama, na kusimama na mwandani wetu, Israel, wamalize Hamas,” aliongeza.

Haya yanajiri huku vuguvugu la Hamas likitisha kuua mateka katika ukanda wa Gaza.

Vita hivi vimesababisha zaidi ya maafa 1,600 kufikia sasa.

Haya yanajiri huku Kenya ikichukua msimamo tofauti na Umoja wa Afrika (AU) kuhusu vita hivyo.

“Kenya inaungana na ulimwengu kwa umoja wa Israel na inakashifu ugaidi na mashambulizi kwa wananchi wa taifa hilo wasio na hatia,” Rais William Ruto alisema kupitia taarifa aliyochapisha katika akaunti yake rasmi ya X.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa AU, Bw Moussa Faki amekinzana na Rais Ruto kuhusu ni taifa lipi linafaa kulaumiwa kwa machafuko hayo.

“Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika anakumbuka kuwa wananchi wa Palestina walinyimwa haki za kimsingi hasa zile za taifa huru,” ilieleza sehemu ya taarifa ya AU.

Hata hivyo, Rais Ruto na Bw Faki waliungana kwa kauli moja kuhusu kusitishwa kwa mashambulizi ya pande zote.

  • Tags

You can share this post!

Mama wa Taifa avalia mavazi ya bei ghali siku ya Utamaduni

Maswali yaibuka Kipchoge kukawia kupongeza chipukizi...

T L