• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 4:50 PM
Odinga aitaka idara ya polisi na mahakama kufanya hima kuangazia suala la watoto kutekwa nyara na kupatikana wameuawa kinyama

Odinga aitaka idara ya polisi na mahakama kufanya hima kuangazia suala la watoto kutekwa nyara na kupatikana wameuawa kinyama

Na MASHIRIKA

KIONGOZI wa ODM Raila Odinga ameitaka idara ya polisi (NPS) na mahakama kufanya kila wawezalo kuangazia kero ya watoto kutekwa nyara na kupatikana wameuawa kikatili.

Katika siku za hivi karibuni, visa vya watoto kupotea, kuibwa na kutekwa nyara kisha wanapatikana wameuawa vimeonekana kuongezeka.Baadhi ya washukiwa wametiwa nguvuni, wengine kufikishwa mahakamani, Idara ya Upelelezi wa Uhalifu na Jinai (DCI) ikiendeleza uchunguzi.

Bw Odinga amesema, ongezeko la visa hivyo na maafa ya watoto, vimekita mizizi na kutia taifa wasiwasi.“Watoto wanatolewa wakiwa katika maeneo ya kucheza – nyanjani, wakielekea ua kutoka shuleni, maeneo ya kuabudu na pia nyumbani kwao, wanatekwa nyara na watu wazima halafu wanawaua kinyama.

“Wasichana na kina mama wanaondolewa uhai na wapenzi, bwana zao na hata wazazi. Matukio ya aina hii hayakubaliki wala kuruhusiwa kamwe,” akasema kiongozi huyu wa ODM.Akiitaka idara ya polisi kuwajibika, Bw Odinga alisema inapaswa kuhakikishia Wakenya na taifa kwa jumla watoto, wasichana na kina mama ni salama.

“Maafisa wa polisi wahakikishie Wakenya hakuna mtu atakayeteka nyara watoto na wasichana na kuwaua,” akasema Waziri huyo Mkuu wa zamani.Bw Odinga alitoa kauli hiyo, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, akielezea hisia zake kuhusu kero na ongezeko la visa vya watoto kutekwa nyara na kupatikana wameuawa kikatili.

Kwa upande wa idara ya mahakama, ameitaka kuhakikishia Wakenya wanapata haki hasa katika kesi za mauaji.Bw Odinga alisema haki kwa waathiriwa inachukua muda mrefu kupatikana, jambo linalowaongezea machungu.

“Haki inapokawia kupatikana, uchungu unawazidi. Idara hizi mbili (ya polisi na mahakama), zihakikishie Wakenya kupata haki ili kuondokea uwendawazimu unaoshuhudiwa,” Bw Odinga akasisitiza.

Mwishoni mwa juma lililopita, visa vya zaidi ya watoto kumi kutekwa nyara na kupatikana wameuawa kinyama, viliripotiwa na kugonga vichwa vya vyombo vya habari.Wakati hayo yakiri, kesi ya Sharon Otieno, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, ilirejelea kuskizwa mwezi huu, Julai 2021, tangu kuuawa kwake 2018.

Gavana wa Migori, Okoth Obado na wafanyakazi wake kadha wanahusishwa na mauaji hayo.Awamu ya pili ya kesi hiyo itaendelea Agosti 2021 na ya tatu baadaye mwakani, Desemba.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge aomba msaada wa Rais kusaidia wahasiriwa wa mkasa wa...

Serikali ya Kaunti ya Kisumu yazika miili 61 iliyokosa...