• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:12 PM
Onyonka avuliwa wadhifa wa Ford Kenya kwa kuunga Raila

Onyonka avuliwa wadhifa wa Ford Kenya kwa kuunga Raila

Na CHARLES WASONGA

MBUNGE wa Kitutu Chache Kusini Richard Onyonka amevuliwa wadhifa Naibu Kiongozi wa Ford Kenya katika mabadiliko yaliyofanywa juzi katika Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wake (NDC)

Jina la Bw Onyonka, ambaye amekuwa akipigia debe azma ya urais ya Kiongozi wa ODM Raila Odinga, halikuorodheshwa miongoni mwa maafisa wapya wa Ford Kenya yaliyochapishwa magazetini jana. Ford Kenya ni mojawapo ya vyama tanzu katika muungano wa One Kenya Alliance (OKA)

Walichaguliwa katika kongamano hilo la NDC, lililofanyika Novemba 4, 2021, katika ukumbi wa Bomas of Kenya, Nairobi. Wadhifa wa Naibu Kiongozi wa Ford Kenya umemwendea Bi Millicent Anyango Abudhu ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu Katibu Mkuu baada ya kutimuliwa kwa mbunge wa Tongaren Simiyu Eseli.

Katika kongomano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Bomas, Nairobi wajumbe wapatao 1,500 Seneta wa Bungoma Moses Wetang’ula alidumisha wadhifa wake kama Kiongozi wa kitaifa wa Ford Kenya. Naye Mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa alichaguliwa kwa kauli moja kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Wadhifa huo zamani ulishikiliwa na Dkt Eseli ambaye pamoja na mwenzake wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi walijaribu kumng’oa Bw Wetang’ula mamlakani mwaka jana. Dkt Simiyu na Bw Wamunyinyi waliongoza mkutano waliodai ni wa Kamati Kuu ya Ford Kenya katika mkahawa mmoja Nairobi na kutangaza kung’oa kundi la Wetang’ula.

Mirengo hiyo miwili ilivutana hadi mahakamani kuu ambapo jaji aliamua kuwa kundi la Bw Wetang’ula ndilo halali.

You can share this post!

Shirika lataka sera za wahudumu melini

Hatima ya Ruto kuamuliwa katika NDC ya Jubilee Novemba 30.

T L