• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 11:05 AM
Paul Pogba arejea Juventus baada ya kuondoka Man-United

Paul Pogba arejea Juventus baada ya kuondoka Man-United

Na MASHIRIKA

KIUNGO Paul Pogba sasa atakuwa miongoni mwa wanasoka wanaodumishwa kwa mshahara wa juu zaidi katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) baada ya kuagana tena na Manchester United na kurejea kambini mwa Juventus.

Pogba, 29, alibanduka ugani Old Trafford mwishoni mwa msimu jana, miaka sita baada ya kutokea Juventus kwa Sh12 bilioni. Nyota huyo raia wa Ufaransa aliwahi tena kusakatia Man-United kati ya 2011 na 2012 kabla ya kuyoyomea Italia kuvalia jezi Juventus (2012-2016).

Kwa mujibu wa gazeti la Dello Sport nchini Italia, Pogba atakuwa akila mshahara wa Sh888 milioni kwa mwaka, malipo hayo yakimweka katika nafasi ya tano kwenye orodha ya masogora wanaopokea ujira mnono zaidi katika Serie A.

Atakuwa akisoma migongo ya Matthijs de Ligt wa Juventus (Sh1.42 bilioni), Alexis Sanchez wa Inter Milan (Sh1.18 bilioni), Adrien Rabiot wa Juventus (Sh1.07 bilioni) na Romelu Lukaku (Sh902 milioni). Lukaku, 29, alirejea Inter kwa mkopo muhula huu baada ya kushindwa kutamba kambini mwa Chelsea.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Vipusa wa Ufaransa wakomoa Italia na kuwapa onyo wapinzani...

Kibicho ataka UDA iwakome machifu

T L