• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 11:05 AM
Pokot Magharibi KCSE yaendelea vyema maeneo hatari usalama ukiimarishwa

Pokot Magharibi KCSE yaendelea vyema maeneo hatari usalama ukiimarishwa

NA OSCAR KAKAI

MTIHANI wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) 2023, katika Kaunti ya Pokot Magharibi ulianza vyema Naibu Kamishna Kaunti Ndogo ya Pokot Magharibi Wycliffe Munanda, akiongoza kusimamia ufunguzi rasmi wa kontena yenye karatasi za mitihani Mjini Kapenguria.  

Bw Munanda alikuwa aliandamana na Mkurugenzi wa Elimu Pokot, Bw Simon Wamae.

KCSE ilianza kote nchini mapema Jumatatu, Novemba 6, 2023 usalama ukiimarishwa ndani nam nje ya vituo vya kufanyia mitihani.

Maeneo Pokot yanayoshuhudia utovu wa usalama, Bw Munanda alisema maafisa wa polisi wameshika doria kila mahali kuhakikisha mitihani inafanyika bila matatizo.

Hata hivyo, kufuatia mvua kubwa inayoshuhudiwa Pokot sawa na maeneo mengine nchini, inahofiwa usafirishaji mitihani huenda ikatatizika kutokana hali mbovu ya barabara.

Kamishina Munanda alisema mikakati kabambe imewekwa kuhakikisha mitihani inafika shuleni au vituo vya kuandika wakati ufaao.

Afisa huyo alitoa onyo kali kwa watakaopatikana kushiriki visa vya udanganyifu au wizi wa mitihani, akisema watadhibiwa kisheria.

“Tunatarajia zoezi hili kufanyika vyema na kwa mazingira bora,” Bw Munanda alisema.

Kwa upande wake Bw Wamae, alikiri usafirishaji mitihani huenda ukakumbwa na changamoto kufuatia mvua kubwa inayonyesha Pokot.

“Nina furaha kuripoti kwamba Pokot kufikia sasa haijaandikisha kisa chochote cha watahiniwa wa kike kujifungua,” akasema afisa huyo wa elimu.

Kuhusu usalama kuimarishwa, Kamanda wa Polisi Kaunti Ndogo ya Pokot Magharibi, Kipkemoi Kirui alisema kuwa vikosi vya usalama vikiwemo maafisa wa kijeshi (KDF), wale wa kupambana na ghasia (GSU), na wanaokabiliana na wizi wa mifugo(ASTU) vimetumwa katika maeneo hatari ya Turkwel na Chesegon.

Aidha, kila kituo cha mitihani kina maafisa wawili wa usalama.

Pokot Magharibi ina jumla watahiniwa 15, 478 ambao wanafanya KCSE 2023, wakiwemo 69 waliojiandikisha kama watahiniwa binafsi.

  • Tags

You can share this post!

Mwanafunzi mjamzito Nakuru kufanyia KCSE hospitalini

Mashabiki wa Shabana waweka historia kwa kujaza uwanja wa...

T L