• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Rigathi Gachagua aahidi kuwaambia wakazi wa Mathira ‘kiongozi bora wa kunirithi’

Rigathi Gachagua aahidi kuwaambia wakazi wa Mathira ‘kiongozi bora wa kunirithi’

NA SAMMY WAWERU

MBUNGE wa Mathira, Rigathi Gachagua ameahidi wakazi wa eneobunge hilo kwamba atawasaidia kusaka kiongozi atakayemrithi.

Hii ni baada ya Naibu Rais Dkt William Ruto kumteua awe mgombea mwenza wake katika kinyang’anyiro cha urais.

Analenga kuhakikisha atakayemrithi atatoka chama chao cha United Democratic Alliance (UDA) kilicho ndani ya muungano wa Kenya Kwanza pamoja na vyama vya Amani National Congress (ANC), na Ford-Kenya miongoni mwa vyama vingine.

“Mimi ninaenda Nairobi na nitawasaidia kutafuta kiongozi ambaye atanirithi, aendeleze miradi ya maendeleo niliyoanzisha,” Bw Rigathi akasema akizungumza katika eneo la Mathira.

Rigathi alichaguliwa mbunge eneo hilo 2017, kupitia chama cha Jubilee.

“Kile ambacho hatutafanya kama wakazi ni kuchagua Azimio, Jubilee au Narc-Kenya eneobunge la Mathira,” akasema.

Mbunge huyo alisema UDA itatoa tangazo la wanaomezea mate wadhifa wake kujitokeza, wapigwe msasa na mmoja kuteuliwa.

“Naibu Rais amenipa kazi, tuna imani atachaguliwa rais Agosti 9 hivyo basi tusimwangushe,” akaelezea, akihimiza wenyeji kupigia kura Kenya Kwanza katika uchaguzi mkuu ujao.

Mathira ni miongoni mwa maeneo yanayounda Kaunti ya Nyeri, ndani ya Mlima Kenya.

  • Tags

You can share this post!

Baadhi ya wakazi wa Thika washerehekea baada ya Karua...

Akina mama wasababisha msongamano Nakuru wakisherehekea...

T L