• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 10:55 AM
Sarakasi Gavana Mwangaza akijadiliwa katika bunge la Seneti

Sarakasi Gavana Mwangaza akijadiliwa katika bunge la Seneti

NA MARY WANGARI

GAVANA wa Meru Kawira Mwangaza ambaye kesi ya kutimuliwa kwake ilianza kusikilizwa Jumanne, amemulikwa kwa kuajiri jamaa wake watatu kusimamia kituo cha matibabu ya kansa licha ya kukosa elimu katika fani hiyo ya matibabu.

Seneti ilisikiliza kwamba gavana huyo alimchukua dada yake, nduguye na shemeji wake wa kiume kuenda kwa ziara ya mafunzo nchini China ili kupata picha ya namna ya kuweka vifaa katika kituo cha kutibu wagonjwa wa saratani.

Kilichowashangaza maseneta ni kwamba barua kutoka kwa gavana iliwarejelea watatu hao kuwa ni “wataalamu wa kansa”. Kikao hicho cha maseneta wote kiliongozwa na Spika Amason Kingi.

‘Kosa’ hilo kwa mujibu wa madiwani wa Meru ni mapendeleo ya kifamilia na ukiukaji wa kimaadili.

“Aliwatuma watu wa familia kama “kikosi cha wataalamu” kukagua vifaa vya matibabu nchini China,” mashtaka dhidi ya Bi Mwangaza yanasema.

Wakili Mkuu Muthomi Thiankolu, mmoja wa mawakili wawili wa Bunge la Kaunti ya Meru alishangaa ni kwa nini gavana aliamua kuwaacha nje wataalamu wa vifaa vya matibabu.

“Dada yake ndiye aliye na elimu ya kiwango cha juu kwa wote watatu, akiwa na stashahada (diploma) ya masuala ya dawa. Mbona akawaacha madaktari bingwa wa kansa, wataalamu wa mashine na wengineo wenye ufahamu wa kansa?” akauliza wakili Thiankolu.

Katika kipindi cha miaka minane, wakazi wa Meru wana hatari ya asilimia 0.32 kupatikana na kansa, kwa mujibu wa jarida la British Journal of Healthcare and Medical Research.

Nao utafiti wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) unaonyesha asilimia tano ya wagonjwa wa kansa katika kituo hicho ni wa kutoka Meru. Kaunti ya Nairobi inaongoza ikifuatwa na Kiambu, na Murang’a.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Waliokuwa wamestaafu waoga na kurudi katika soko la ajira

Mabunge ya Kenya, Zambia yapigia debe chama chao cha...

T L