• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Sifuna akemea Jubilee kwa kutisha kujiondoa Azimio

Sifuna akemea Jubilee kwa kutisha kujiondoa Azimio

NA CHARLES WASONGA

KATIBU Mkuu wa ODM Edwin Sifuna amedai kuwa chama cha Jubilee kilifeli kuleta idadi tosha ya kura kutoka eneo la Mlima Kenya, akisema hiyo ndiyo ilisabisha kushindwa kwa Raila Odinga.

Akirejelea ripoti kwamba wabunge wametisha kuwa chama hicho kitajiondoa kutoka muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya, Bw Sifuna ambaye pia ni Seneta wa Nairobi alisema kuwa Jubilee ilileta kura 490,000 pekee ilhali iliahidi jumla ya kura 2 milioni.

“Ni nyinyi Jubilee ndio mliotuangusha kwa kufeli kutimiza ahadi mliotoa kwamba mngemwezesha Raila kupata kura milioni mbili kutoka Mlima Kenya. Kura 490,000 mlizoleta hazikutosha kumwezesha Baba (Raila) kuingia Ikulu. Sasa msitoe vitisho,” akasema Bw Sifuna.

Wiki jana, wabunge na maseneta wa Jubilee walitisha kugura Azimio baada ya kukerwa na hatua ya kuondolea kwa jina la Seneta wa Isiolo Fatuma Dullo kutoka orodha ya wawakilishi wa Azimio katika Tume ya Huduma za Bunge (PSC).

Nafasi yake ilipewa Seneta wa Nyamira Okongo Omogeni (ODM), hatua ambayo iliwakera wabunge na maseneta wa Jubilee.

Hata hivyo, aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Njunjiri Wambugu alisema kuwa yeye alipoteza kiti chake kwa sababu ya kumuunga mkono Bw Odinga, licha ya kiongozi huyo wa ODM kuvuna kura chache katika kaunti yake ya Nyeri.

  • Tags

You can share this post!

Ufugaji kuku unayumbishwa na gharama ya juu, asema mkuu wa...

Karua asuta serikali kuhusu udikteta

T L