• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:36 PM
Takataka iliyowakera wakazi eneo la viwandani na mtaani wa mabanda laondolewa

Takataka iliyowakera wakazi eneo la viwandani na mtaani wa mabanda laondolewa

Na SAMMY KIMATU

NAIROBI

TAKATAKA iliyorundikana katika mtaa mmoja wa mabanda South B, kaunti ya Nairobi na kuwakera wakazi kwa majuma kadhaa hatimaye imeondolewa.

Awali, wakazi katika mtaa wa mabanda wa Kaiyaba ulioko kwenye lokesheni ya Landi Mawe, kaunti Ndogo ya starehe walilalamika baada ya uvundo na ongezeko la nzi kuvamia vibanda vya vyakula.Jaa hilo la taka lilikuwa kando na steji ya matatu ya Kayaba mkabala wa barabra ya Entreprise kwenye Eneo la Viwanda.

Kando na wakazi kutoka mtaa wa Kayaba kulalamika, wengine waliotoa sauti zao ni pamoja na wafanyabiashara wa bodaboda na abiria wanaotumia barabara ya Entreprise.

“Kusema kweli takataka ilikuwa imekaa kwa siku nyingi bila kukondolewa wakati huu. Nzi walikuwa wanavamia vibanda vya vyakula mtaani na taka nyingine kufunga sehemu ya barabara ya Entreprise,” Bw Onesmus Kalei, mwanakamati wa Nyumba Kumi mtaani Kayaba akaambia Taifa Leo.

Chifu wa eneo hilo, Bw Mulandi Kikuvi alisema wakazi walikuwa wamepiga ripoti katika ofisi yake kuhusu jaa la taka lililowakera wengi katika steji ya Kaiyaba ndiposa hatua ya haraka ikachukuliwa.Mwishoni mwa wiki, tingatinga na malori ya idara ya Huduma za Jiji la Nairobi (NMS) yalishinda mahali pa kutupa taka yakizoa na kuzipeleka Dandora.

Jaa hilo la taka la steji ya Kayaba hutumiwa kutupia taka na wakazi wa mtaa wa mabanda wa Kayaba, Mtaa wa mabanda wa Maasai na wenzao wa mtaa jirani wa Hazina.

 

Picha/SAMMY KIMATU

“Baada ya mitaa ya mabanda kukosa mahali maalumu pa kukusanyia takataka ili iwe ikichukuliwa kutoka eneo lililotengwa na kupelekwa mtaani Dandora, serikali ya kaunti ilitenga eneo lililoko karibu na steji ya Kayaba kuwa ndilo la kutupia taka,” Bw Azangu asema.

Baada ya malori kuzoa taka zote, eneo hilo limerudia hadhi yake ya usafi na watu wakafurahi.Kadhalika chifu Mulandi amewaomba wakazi wa mitaa husika kuwa makini wanapomwaga taka badala ya taka kutupwa barabarani.

“Ni jukumu la kila mmoja wetu kuzingatia usafi wa mazingira. Kwa hivyo, msimwage uchafu barabarani ili mwajali wenye kutumia barabara ya Entreprise,”chifu Mulandi akaonya.

Picha/SAMMY KIMATU
  • Tags

You can share this post!

Wakenya KPA wafundisha klabu za Malawi jinsi ya kucheza...

Ondoa gharama ya kununua fatalaiza kwa kujitengezea mbolea...