• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
TALANTA YANGU: Anainukia katika uchoraji vibonzo

TALANTA YANGU: Anainukia katika uchoraji vibonzo

NA PATRICK KILAVUKA

ANAAMINI uchoraji wa vibonzo ni taaluma kwa sababu kuna wanavibonzo ambao wanapata posho kwa kuchora vibonzo magazetini na kubuni vingine vya kidijitali ambavyo vimetawala sasa vipindi vya runinga kama Akili kids, Ubongo Kids, Spiderman, Super Strikers, Tom and Jerry, Sponge Bob miongoni mwa vingine vinavyotazamwa.

Hususa anapovitazama kwenye magazeti ya Taifa Leo, Daily Nation na kadhalika hupata, mshawasha wa kuwa na kiu ya kujitahidi kuchora, kuelimisha, kuhamasisha na kutumbuiza kuvipitia.

Hayo ni kwa mujibu wa Bramwel Okemwa,11, mwanafunzi wa Gredi ya tano, Shule ya Msingi ya Young Achivers, Nairobi.

Yeye ni mwanambee katika familia ya watoto wawili wa Bw Jeremiah Arisa na Bi. Nancy Kerubo.

Alianza kuchora vibonzo akiwa na miaka tisa ambapo alikuwa anatiwa hamasa na rafiki yake Renson Fundi ambaye walikuwa wanachora naye kila uchao baada ya kumaliza kazi za ziada shuleni.

Wakati huu wa likizo, amekuwa akichora na mwanafunzi Emmanuel Lobarido,11,gredi ya sita muhula ujao wa Shule ya Msingi ya Bohra, Westlands ambaye anakiri kwamba, vibonzo kwake ni muhimu kwa manufaa ya elimu, kutumbuiza, kuchangamsha na kusawazisha mawazo akiwa na mfadhaiko.

Mwanavibonzo Okemwa alifunguka kiakili kuchora vibonzo baada ya kuvitazama kwenye vipindi vya runinga kama Spiderman, Sponge Bob, Tom And Jerry, World Kratts pamoja na kusoma magazeti ya Taifa Leo, vitabu vya hadithi vilivyosanifishwa na picha za michoro.

Umuhimu wa vibonzo licha ya yeye mchoraji wavyo ni kwamba, vinaangazia hali halisi za maisha na huwa vinaelimisha, changamsha ubongo, furahisha na huongezea maarifa ya ubunifu hususa wakati huu mtaala wa umilisi umekuwa wa maana. Pia, kuna kupata uzoefu wa uchoraji ambao unajiumbua ndani mwake na kuwa na tumaini kwamba, michoro ya vibonzo itamvunia mapato usoni.

Mwanavibonzo chipukizi Bramwel Okemwa. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Anasema vile vibonzo ambavyo anavihusudu ni vya Sponge Bob vya Teen Titans. Anadokeza kwamba utazamaji wa vibonzo umeimarisha uwezo na upevu katika masomo ya Hisabati na Sayansi kwa kuwa na ubunifu na kupata mifumo ya uchoraji.

Yeye huvutiwa pia na ulimbwende wa kupaka rangi mbalimbali kwenye vibonzo.

Wazazi wake anawataja kuwa wa wana msaada mkubwa katika kukuza talanta yake kwani wanamsambazia malighafi yafaao katika kufanikisha usanii wake.

Angependa kuwa daktari mbali na msanii wa uchoraji.

Uraibu wake ni kusoma vitabu vya hadithi hususa vilivyo na vibonzo pia kwa sababu hutoa taswira ambazo hupelekea uelewa wa stori kuwa rahisi.

Ushauri ni kwamba, wanafunzi wanaweza kuimarisha vipaji zaidi iwapo wazazi watawashika mkono kwa kuwapatia malighafi inayohitajika na watie bidii ya mchw haswa wakati huu wa mfumo wa umilisi wa mtaala ambao unahimiliwa na utendakazi kwa wanafunzi.

You can share this post!

Achani ataka wapinzani wake kutoendeleza siasa za ukabila

PAUKWA: Bahili aokolewa na msamaria mwema

T L