NA MAUREEN ONGALA
AFISA wa kike katika serikali ya Kilifi ameuawa kwa kudungwa na kifaa cha nyumbani leo Alhamisi.
Afisa Mkuu wa Uchumi wa Baharini Bi Rahab Karisa ametendewa unyama huo na mjakazi wake ambaye amemdunga kisu asubuhi na mwili wake tayari umepelekwa katika mochari ya Hospitali ya Rufaa ya Kilifi.
Kamanda wa Polisi Kaunti ya Kilifi Bi Fatuma Hadi amethibitisha tukio hilo la kuhuzunisha.
“Kwa sasa majeraha yanayoenekana ni ya kisu lakini tunaendeleza uchunguzi na tutajua mengi baada ya mwili kufanyiwa upasuaji,” amesema kamanda Hadi.